MRADI WA VIUNGO KUFUNGUA FURSA KWA WAKULIMA NA KUONGEZA LISHE BORA.

 



📌MUHAMMED KHAMIS.

Baadhi ya Wananchi wa Shehia mbali mbali Unguja wameleza matarajio yao juu ya ujio wa mradi wa Viungo kuwa utakwenda kufungua fursa kwa wakulima pamoja na kuongeza kipato sambamba na upatikanaji wa lishe bora na uwekaji wa hakiba dhidi yao.

Wameyasema hayo katika shehia ya Bandamaji mkoa wa kaskazini Unguja na baadhi ya shehia nyengine mbali walipokua wakipatiwa elimu juu ya mradi huo utakao jikita katika kilimo cha matunda,mbogamboga pamoja na viungo na kufanyika zaidi ya shehia 50 za Unguja na Pemba.

Wamesema kwa miaka mingi wamekua wakijishughulisha na shughuli za kilimo tofauti lakini hadi leo hii bado hawajafikia malengo yao ipasavyo.

 Mmoja miongoni mwa wananchi hao Kidume Juma amesema licha ya kuwa  shughuli kubwa kwao ni kilimo lakini hadi leo hii bado wakulima walio wengi wamebaki kuwa masikini wanati wao ndio walipaswa kuwa kama walivyowakulima wengine ulimwneguni.

Amesema imefika wakati wakulima katika eneo hilo na maeneo mengine wanafanya shughuli hizo kama mazoea lakini si kwa kutegemea mafanikio kama wengine.

 ‘’Kuna wakati tunajikuta shamba zima la mananasi ama bidhaa nyengine baad aya kumaliza mavuno tumekula hasara au tunapata kile tulichokitoa tu kwa ajili ya uandaaji wa shamba na mambo mengine huku tukiwa tumepoteza nguvu na muda mwingi.

Nae Chapa Mkali Juma amesema licha ya uwepo wa changamoto hio lakini pia wamekua wakikabiwa na tatizo kubwa la uhaba wa masoko kwa bidhaa zitokananzo na kilimo chao.

Amesema katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar wananchi walio wengi hususani mashinani vijijini wamehamaisika na kilimo lakini wamekua wakikata tamaa wanapoona bidhaa zao zinakwenda sokoni bila kununuliwa kama walivotarajia.

Ameeleza kuwa kikawaida mkulima hutumia nguvu nyingi kuzalisha mazao lakini matunda ya nguvu hizo ni madogo sana na yasioendana na uhalisia wa kazi wenyewe.

 ‘’Kwa mfano ulanguzi unaofanywa na baadhi ya watu masokoni wanaojiita madalali kushusha bei kwenye mazao yetu kwa sababu tofauti  ikiwemo kukosa ubora wa bidhaa huku wao wakiuza bei za juu kwa wanunuzi suala hili linatuumiza sana na lazima lifanyiwe kazi’’ameongezea.

 Akitolea ufafanuzi wa changamoto hizo afisa Afisa maendeleo biashara  kutoka mradi wa viungo  Zanzibar  Mwanaidi Mussa Shembwana alisema katika jamii kumekuepo na wakulima wengi wanaoendelea kulalamikia kukosa manufaa ya jasho lao kutokana na sababu tofauti.

 Akitaja miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na wakulima kutojua mbegu sahihi za matunda ambazo zingeweza kuwasaidia kupata kipato zaidi kufuatia uhitaji wa wananchi sokoni.

Amesema kwa mfano hadi leo hii katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar licha ya kuwa ardhi yake kukubali kilimo cha nanasi lakini bado wakulima hawana taaluma ni aina gani ya matunda hayo yanahitajika zaidi katika masoko ya ndani na ya kimataifa.

 Sambamba na hayo amesema  wakulima wanahitaji kupatiwa elimu ni wakati gani na sahihi kwao kufanya kilimo na mbegu gari ni bora zaidi  kwa kuwa kuna mazingira kikawaida si sahihi kuazisha baadhi ya vilimo kutokana na kukosa uhitaji wa bidhaa katika kipindi hicho.

Kuhusu suala la uhaba wa masoko aliwataka wakulima hao kuamini kuwa kila bidhaa iliobora inauzika sokoni hivyo kupitia mradi huo watahakikisha wanufaika wote wale iwe wa vikundi au mtu mmoja mmoja wanazalisha bidhaa bora na zenye viwnago vya kimataifa.

‘’Kwa hili la masoko naomba niwatoe wasiwasi tuna wenzetu ambao wapo Canada jukumu lao kwa kushirikiana na sisi nikuhakikisha tunapata masoko ya kimataifa kwa bidhaa zote zinazozalishwa Zanzibar kupitia mradi huu na ninaamini mutaweza’’aliongezea.

 Awali afisa  fedha kupitia mradi huo  Agnes Nicodemas Msengi amesema licha ya mradi huo kunufaisha wakulima kupitia kilimo lakini pia utasaidia wakulima kuwa na utaratibu maalumu wa kujiwekea akiba.

 Amesema kuna mkakati maalumu wa taaluma ambayo watapewa wakulima wote hususani wenye vikundi vya akinamama waweze kuweka akiba ya kujipatia mikopo katika benki mbbali mnali hapa Zanzibar.

 Mradi wa huu wa viungo ni wa miaka mine na unaendeshwa na taasisi  ya People development forume,Community forest in Pemba pamoja na TAMWA-Zanzibar kwa kuufadhiliwa na umoja wa Ulaya chini ya usimamizi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.


01.Baadhi ya washiriki wa mkutano wa utowaji elimu kuhusu mradi wa Viungo katika shehia ya Bandamaji mkoa wa kaskazini Unguja wakifuatilia taarifa za utolewaji wa elimu kuhusu kilimo cha mboga mboga na matunda pamoja na viungo.

                       
Picha ya pamoja kwa washiriki wa mkutano wa utolewaji elimu dhidi ya mradi mpya wa viungo unaofadhiliwa na umoja wa Ulaya  (EU) kwa usimamizi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Baadhi ya akinamama kutoka shehia ya Bandamaji mkoa wa kaskazini Unguja wakionesha karatasi ilioashiria umuhimu wa kueka hakiba ambayo ni miongoni mwa ajaenda kuu ya katika mradi wa viungo.

Miongoni mwa washiriki wa mkutano wa utolewaji elimu kuhusu mradi wa viungo ambao ni vijana wakifuatilia kwa makini elimu juu ya mradi huo na umhimu wa ushiriki kwa vijana katika mradi huo.

 


 





Post a Comment

0 Comments