TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA YAKABIDHIWA MAGARI MATANO NA KOMPUTER 70.

 

📌DEVOTHA SONGORWA.

 WAZIRI wa Kilimo, Profesa, Adolf Mkenda, amekabidhi magari matano na komputa 70 kwa warajisi wa mikoa lengo likiwa kuendeleza vyama vya ushirika na kuimalisha utendaji katika vyama hivyo.

 Makabidhiano hayo yamefanyika leo januari 06,2021  katika viwanja vya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC),jijini Dodoma.   

 Waziri Nkenda amesema serikali imedhamiria kurudisha heshima na imani iliyokuwa imepotea kwa  ya watu kutokana na madhaifu ambayo yamekuwa yakijitokeza kama wizi, ubadhirifu wa mali za umma na mfumo mbovu wa uongozi kwenye vyama hivyo.

Amesema anatambua kazi kubwa inayofanywa na vyama vya ushirika ikiwa ni pamoja na kuunganisha nguvu katika sekta ya uzalishaji ikiwemo kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kama wavuvi na wakulima.

"Tunataka kuhakikisha ile heshima ya mwanzo inarudi ili watu wengi hasa wakulima kujiunga na vyama vya ushirika na kukuza soko letu la mazao kimataifa," alisema Profesa Mkenda.

 Amesisisitiza kumekuwa na baadhi ya watu ambao wanaichafua taswira ya vyama vya ushirika kutokana na wizi na utendaji mbovu wa kazi, hivyo aliwataka viongozi kwenda kushughulikia changamoto hizo.

 Amesema serikali itahakikisha inashirikiana vyema na vyama vya ushirika ikiwa ni pamoja na kupitia upya sheria ya vyama hivyo ili kuona ni sheria zipi zinakuwa kikwazo kwa baadhi ya watu kushindwa kujiunga.

 “Tutapitia upya sheria ya vyama vya ushirika pamoja na kukomesha wizi na ubadhirifu ili kuhakikisha unakwisha kabisa," alisema.

 

Naye, Mrajisi wa Vyama vya Ushirika ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dk. Benson Ndiege, alimshukuru waziri huyo kwa kukamilisha makabidhiano hayo na kumuomba aendelee kutembelea taasisi hiyo.

 Ndiege amesema tume inaendelea kuhamasisha wanachama wa vyama vya ushirika, kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za vyama vyao na wakati huo akiwahamasisha viongozi kuendelea kutoa huduma zinazotarajiwa na wanachama wao.

Amesema wanaendelea kuimalisha ushirikiano na taasisi zingine za serikali, binafsi na wadau wa ushirika katika kuongeza thamani kwa wanaushirika.

 “Ili kufanikisha yote haya tutahakikisha vyama vinapata viongozi wenye uwezo na weredi kwenye vyama vya ushirika na tutashirikiana na na taasisi zingine za serikali kuazia mikoa ,wilaya mpaka Takukuru,”alisema.

 Ndiege amesema katika kuhakikisha wanadhibiti wizi na ubadhirifu katika vyama hivyo, alisema wamejipanga kuhakikisha wanafanya usimamizi wa mara kwa mara kwenye vyama vya ushirika na kuhakikisha wale wote wanaojihusisha na wizi au ubadhirifu wa mali za ushirika wanawajibishwa ipasavyo.

“Tumejipanga kisawa sawa kuhakikisha kila sekta inakuwa vizuri hatutafumbia macho vitendo vyovyote viovu vitakavyo jitokeza, tupo tayari kufanya kazi na yeyote atakayekiuka maagizo ya tume,” amesema.

Waziri wa Kilimo,Prof.Adolf Mkenda akitoa hotuba leo januari 06,2021  katika viwanja vya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC),jijini Dodoma.   

 

Magari manne yaliyokabidhiwa leo Januari 06,2021kwa warajisi na Waziri wa Kilimo, Profesa, Adolf Mkenda kwa warajisi wa mikoa lengo likiwa kuendeleza vyama vya ushirika na kuimarisha utendaji katika vyama hivyo.

Post a Comment

0 Comments