WAFUGAJI BADILISHENI MFUMO WA UFUGAJI.


📌SALEH RAMADHANI.

Kaimu mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa mifugo kituo cha pwapwa TALIRI  Dokta Aluna chawala ametoa wito kwa wafugaji nchini kubadilisha mitazamo ya ufugaji ya kufuga mifugo kama ziada badala yake wafuge kwa ajili ya biashara.

Hayo yamebainishwa leo wilayani mpwpwa mkoani Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Taasisi ya Utafiti wa Mifugo TALIRI Mpwapwa Dokta Aluna chawala  ambapo amesema wafugaji waliyo wengi wamekuwa wakifuga kwa mazoea  hivyo nivyema kubadilika na kufuga ng'ombe wanaoendana na mazingira yao hasa ngombe hawa aina ya mpwapwa ambao wana vumilia ukame na magonjwa.

"uzalishaji wa kibiashara wa maziwa na nyama ya ng'ombe na uzalishaji malisho bora ya mifugo ni muhimu kabla ng'ombe hajauzwa maana uzalishaji wa vyakula ni muhimu sana kabla ng'ombe hajauzwa au kupelekwa sokoni sambamba na mifumo madhubuti endelevu ya kuzuia na kutibu maradhi mbalimbali ya mifugo" amesema chawala

Dokta Chawala amesma kuwa ng'ombe aina ya mpwapwa ni ngombe  chotara aliye changanywa na damu ya ngombe  kutoka bara la Asia ulaya na wa asili hapa Tanzania  pia ni ngombe anayevumilia ukame na matunzo yake ni ya gharama nafuu na gharama za kutunza ng'ombe jike Tangu anapozaliwa hadi anapokuwa na mimba ni kati ya shilingi laki Tisa hadi Millioni na laki mbili  na matokeo haya ya utafiti yamewezesha wafugaji kuunda vikundi na kuuza kwa faida.

Adhai dokta chawala  amezihimiza serikali za mitaa kuwasaidia wafugaji  kutumia mbegu za ng'ombe aina ya mpwapwa  zinazosambazwa na kituo cha  taifa cha usariver kilichopo  Mkoani Arusha.

"Ng'ombe aina ya mpwapwa wanafaida kubwa sana maana anavumilia ukame,na magonjwa mbalimbali pia anatoa maziwa mengi na nyama ukilinganisha wa Asili na wale wakisasa,na matunzo yake ni gharama nafuu ukilinganisha na ng'ombe wetu wa Asili na wakisasa" Amesema Chawala.

Naye mwenyekiti  wa chama cha wafugaji Tanzania  Jeremia wambura amewaasa wafugaji kuzingatia chanjo  ilikuboresha afya za mifugo yao na wawe na utaratibu kuhifadhi nyasi kwa ajili ya  malisho hasa katika kipindi cha kiangazi.

Aidha mwenyekiti wa chama cha wafugaji  ameizungumzia sekta ya ufugaji kuwa ni sekta  inayoweza kujiendesha yenyewe kama chama wamejipanga kuisaidia wizara ya Mifugo na uvuvi ili iweze kujiendesha yenyewe kwani ni wizara nyeti.

"Sekta ya mifugo ni sekta nyeti na sisi kama chama cha wafugaji Tanzania jimejipanga katika kuhakikisha wafugaji wananufaika na mifugo wanayoihudumia na ukiwa na mifugo yoyote na katika mifugo hiyo Thelusi Moja Lazma awe ng'ombe wa Maziwa" Amesema Wambura.

Nao baadhi ya wafugaji wanaofuga ng'ombe aina ya mpwapwa akiwemo Hassani Tati kutoka Singida Amesema kuwa ng'ombe hao wamemnufaisha sana na kudai kuwa ng'ombe aina ya mpwapwa wanauwezo wa kuzaa kila mwaka ukiwatunza vizuri na wanauwezo wa kutoa maziwa lita kumi kwa Siku.

"Wallah ng'ombe hao ukiwatunza vizuri wanauwezo wa kuzaa kila Mwaka na wanatoa Maziwa Lita kumi kwa Siku, maziwa tu yananipa faida kubwa sana pia maisha yangu nayaendesha vizuri na watoto wangu wanasoma vizuri,lakini ng'ombe hawa hawaitaji sana Tiba useme nigarama sana hapana,lakini Mimi nawaogesha kwa wiki Mara moja tu pia nawashauri wafugaji wote nchini wanunue Ng'ombe wa Mpwapwa Maana wanafaida kubwa sana,Mimi nimeuza siyo chini ya Madume 20 kwa watu mbalimbali ili nao waone faida ya kuwa na ng'ombe hawa" Amesema Tati.

Hatahivyo amewashauri wafugaji wenzake  kubadilisha aina ya  mifugo wanayoifuga na kufuga ng{ombe aina ya mpwapwa  kwani wanafaida kubwa wanaweza kuwaingizia kipato kikubwa kuliko ngombe wa asili kwa kuuza maziwa ambapo yeye huuza lita kumi za maziwa kwa siku.

Post a Comment

0 Comments