WAKUU WA MIKOA KUWENI WALEZI KATIKA SHULE ZA UFUNDI.

 


📌HAMIDA RAMADHAN 

WAZIRI wa Nchi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amewataka Wakuu wa Mikoa hapa Nchini kuwa walezi wa shule za Ufundi  ili kufanya mabadiliko na Mapinduzi makubwa  ya viwanda.

 Waziri Jafo ameseyasema hayo leo Jijini hapa wakati alipokuwa  akiongea na walimu wapya na Wakuu wa Mikoa kupitia njia ya Mtandao ambapo amewataka walimu kuacha kujifungia na badala yake wawashirikishe mafundi mahili waliopo mitaani ili kuleta Mapinduzi ya viwanda kwa wanafunzi na shule zote za ufundi.

 Waziri Jofo amesema shule za ufundi kipindi cha awali zilipoteza hadhi yake na hapakuwa na miundombinu Wala rasilimali Watu Hali za shule hizo zilikuwa mbaya.

 "Shule za ufundi zinawaandaa Vijana kujifunza masuala ya ufundi

Hivyo basi niziagize Halmashauri zote zisimamaie miondombinu ya shule hizo na kuzikarabati kila wakati," amesema Waziri Jafo.

 Aidha amefafanua kwamba jumla ya Shilingi bilioni 16.34 zimetengwa na Serikali kwa ajili ya ukarabati wa shule zote za ufundi ambapo pia jumla ya walimu150 wameajiliwa ili kupelekwa Katika shule hizo.

 "Hivyo basi Niwaagize walimu wote walioajiliwa waakikishe wanakwenda kufanya kazi kwa bidii na umahiri Katika taaluma hiyo ya ufundi hatutaki kusikia habari za kununua Chaki na badala yake shule hizi za ufundi zitengeneze Chaki," .

 Na kuongeza kusema kuwa " Haiwezekani hadi leo bado tunaagiza vijiti vya meno nchini China hii ni aibu wakati tunamiti ya kutosha kwaajili ya kutengeneza mbao," amesema Waziri Jafo.

 

Post a Comment

0 Comments