BASHE AKUTANA NA VYAMA VYA MSINGI SEKTA NDOGO YA CHAI

 


📌HAMIDA RAMADHANI

NAIBU Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amekutana na Vyama vya Msingi 41 vya Sekta ndogo ya Chai lengo likiwa ni kuweka mikakati ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo nchini kutoka Tani 25000 hadi kufikia tani 60000 ifikapo Mwaka 2024.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini hapa  Bashe amebainisha kwamba mikakati hiyo ni pamoja na kuhakikisha wakulima wanapatiwa Pembejeo na uhakika wa masoko kwa njia ya minada.

"Nimekutana  na Vyama vya ushirika kwenye sekta ya Chai ili kuangalia changamoto zinazowakabili lengo likiwa ni kuinua sekta hii muhimu kwa mustakabari wa Maendeleo ya wakulima wetu na viwanda vya kuchakata chai kwa ujumla," amesema Bashe.

Aidha Bashe amesema katika kikao hicho  wameweza kujadaili mfumo wanaotumia wakulima kupata Pembejeo ambapo amewataka wakulima wote nchini kuagiza mbolea kupitia Vyama vyao vya Ushirika iliwaweze kupata kwa punguzo la bei pia kwa mikopo.

Mwaka jana tulifanikiwa kwa kiasi kikubwa lakini mwaka huu tunataka tufanya zaidi angalia kila mkulima apate mbolea kupitia mfumo wa kuchukua mbolea halafu unalipa baada ya siku 180 ambapo katika muda huo Kila mkulima atakuwa amevuna mazao yake inakuwa rahisi kulipa

Kwa Upande wake Mkurugenzi kutoka Bodi ya Chai Tanzania Nicholaus Mauye.Amesema  lengo la kikao hicho ni kuona Maendeleo ya tansinia kupitia mkulima mdogo mdogo wa chai

Amesema Katika kikao hicho changamoto za wakulima na mikakati yao imechukuliwa na kwenda kufanyia kazi ili kukifanya Kilimo cha chai kinakuwa chenye tika kwa wakulima.

Naye Meneja wa Ununuzi wa Mbolea  kwa Pamoja Maduhu Mkonya amesema wamekutana wakulima hao kuhakikisha wanapata mbolea kwa kuagiza  kupitia mfumo huo wa Kilektronik ambao fedha zake mkulima analipa kwa muda wa miezi 6 baada ya kuvuna mazao yake.

Amesema mfumo huo ni kama huba kwani unaendeshwa kwa njia ya Kilektronik ambapo suala la kuchelewa au mbolea kuulizwa kwa bei ya juu haitakuwepo.

Naye Mkulima Santino Mtenda mkulima wa chai na mkonge kutoka Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa  Amesema zao la chai ni zao la kimkakati hivyo wamepata faraja baada ya kuona Serikali inaanzisha minada kwani masomo kwa wakulima yataimalika.

 

Post a Comment

0 Comments