JUHUDI ZA PAMOJA ZINAHITAJIKA ILI KUKUZA MATUMIZI BORA YA MAWASILIANO-DKT, CHAULA.

 

 


 ­čôîFAUSTINE GIMU.

Katibu mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Zainabu Chaula  amesema juhudi za pamoja zinahitajika  kutengeneza ,  mazingira ya kukuza matumizi bora ya mawasiliano  nchini.

Dkt.Chaula amesema hayo jijini Dodoma  katika Kikao cha kujadili Mkakati wa TEHAMA  kwenye  ngazi ya jamii  ikiwemo vituo vya Afya na shule  hapa nchini  ,Tanzania Community  Digitization[TCD]kilichokutanisha wadau mbalimbali wa Mawasiliano.

Juhudi hizi za pamoja zitatusaidia katika kukuza sekta ya mawasiliano zikiwemo ni pamoja na mkongo wa Taifa wa Mawasiliano  hii ni katika kuhakikisha mawasiliano yanafika katika ngazi zote hadi vijijini”amesema.

Aidha,Dkt.Chaula amesema moja ya malengo ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ni kuhakikisha taasisi zote za umma zinapata huduma ya Mawasiliano kwa gharama nafuu ifikapo mwaka 2025 wizara itajipima angalau kufikia asilimia 40%  .

Hata hivyo,Dkt.Chaula amebainisha kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga ni kwa namna gani inahakikisha inafikisha huduma ya mawasiliano  katika maeneo mbalimbali  ambapo wizara imetoa mwelekeo  katika kusambaza huduma ya mawasiliano.

“Ndio maana serikali ina sera ya TEHAMA ya mwaka 2000 na mwaka 2016 serikali ilipitia sera  ili kwendana na mazingira  na maendeleo ya Teknolojia ,lazima tutengeneze mazingira ya Evaluation mwezi uliopita umefanya nini na sasa unafanya nini,na tunatambua mchango wa sekta binafsi katika mawasiliano hivyo tumejipanga katika kuhakikisha sekta ya mawasiliano inasonga  mbele”amesema.

Pia ,Dtk.Chaula amesema vyombo vya Habari vina mchango mkubwa katika kuhabarisha umma juu ya umuhimu wa mawasiliano katika kukuza uchumi wa  nchi.

 Kwa upande wake Mkuu wa mifumo  ya Habari  USA, Desden Wengaa amesema wataendelea kushirikiana na Wizara katika Nyanja mbalimbali za mawasiliano.

“Kwa nanma moja ama nyingine wote tunahusika na jambo hili ,tumejenga mifumo mikubwa TAMISEMI ,kupitia level za halmashauri mpaka level za vijiji ,ili mifumo ifanye kazi vizuri lazima internet connection”amesema.

Mulembwa Munaku   Mkurugenzi wa TEHAMA Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Mkurugenzi wa TEHAMA Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mulembwa Munaku amesema  pamekuwepo na changamoto ya wadau wengi kupeleka huduma ya mawasiliano katika sehemu moja na wengine kukosa huduma hiyo  .

Dkt.Florence Rashidi  mkuu  wa idara ya mawasiliano ya uhandisi na  elektroniki kutoka chuo kikuu cha Dodoma.

Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya  kutoa majukwaa ya  mtandao wa kujifunzia kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari[Shule Direct]  Faraja Nyarandu  amesema mradi huo umekuja kwa muda muafaka katika kukuza sekta ya mawasiliano nyanja za elimu huku mkuu  wa idara ya mawasiliano ya uhandisi na  elektroniki kutoka chuo kikuu cha Dodoma Dkt.Florence Rashidi akibainisha wamejipanga kushirikiana

 

Post a Comment

0 Comments