KOFFI OLOMIDE: NITAENDELEA KUWA KARIBU NA WATANZANIA

 ðŸ“ŒHABARI MAELEZO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi akiteta jambo na mwanamuziki galacha duniani katika muziki wa rhumba, Koffi Olomide aka Mzee ya Mboka, walipokutana usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam ambapo mwanamuziki huyo alikuwa nchini kutumbuiza chini ya mwaliko wa kampuni ya Prime Time Promotions na Clouds Intertainment.



Dkt. Abbasi ametumia muda huo kumshukuru mkongwe huyo kwa kuitangaza Tanzania mara kwa mara ikiwemo kushirikiana na wanamuziki vijana wa hapa nchini kuinua na kuutangaza muziki wao. Koffi aliahidi kuendelea kusaidia kukuza vipaji vya Tanzania akisema: "Dar es Salaam na Tanzania mimi ni kama nyumbani, nitaendelea kuwa nanyi karibu."

Post a Comment

0 Comments