NCHI WANACHAMA WATOE MICHANGO KUWEZESHA SHUGHULI ZA MAHAKAMA.

 

📌DEVOTHA SONGORWA.

MAHAKAMA,ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACJ) imezitaka  Nchi wanachama wa mahakama hiyo kutoa michango yao ipasavyo ili kuondoa changamoto zinazowakabili mawakili na wanananchi na kusababisha mlundikano wa kesi.

 Hayo yalisemwa leo na Mrajisi Mkuu wawa mahakama hiyo Yufnalis Okubo katika  mazungumzo maalumu na gazeti hilibambapo alisema ukosefu wa fedha za kuendesha shughuli za mahakama umekuwa ukidhoofisha utendaji kazi.

 "Mahakama bado haijulikani inafanya nini wanachanganya na ile  ya AU kwa sababu wote tupo Arusha na tunakwama kwa sababu hatuna fedha ya kuzunguka Nchi zote sita za Jumuia kutoa elimu wakati mwingine wanachama wanasema hawana hela ifike wakati nchi hizi zione umuhimu wa mahakama kufanya kazi katika hali ya ubora,"alisema Mrajisi huyo.

 Pia Amesema bado wananchi hawana elimu kuhusu uwepo wa mahakama hiyo na majukumu yake akisema kwamba ilianzishwa kwa lengo kuwasaidia kupata haki na ufumbuzi wa malalamiko yako pindi Serikali husika inapokiuka Sheria zake.

 "Court hii iliteuliwa kwa ajili yao japo baadhi wanashindwa kuzitofautisha kazi zetu na mahakama nyingine na siyo kila kesi inaletwa hapa ila ni zile zinazohusu Serikali kukiuka Katiba ya Jumuia ya Afrika Mashariki au Serikali kuvunja Sheria yake yenyewe na kuumiza wananchi, kampuni inayofanya Biashara miongoni mwa Nchi za Jumuia hii anaweza kufungua kesi dhidi ya Serikali husika endapo haikutendewa haki au mtu yeyote anaweza kuifungulia mashtaka,"alisema Mrajisi huyo.

 Okubo  akizungumzia mikakati ya mwaka 2021 alisema wanatarajia kumaliza kesi nyingi zilizosalia na kuhakikisha Majaji  wote wa mahakama wanaishi mkoani Arusha kwani hulazimika kuhudhuria mahakamani Mara moja kwa mwezi kutokana na kutokuwa na makazi maalumu hapa nchini hivyo kusababishwa kuchelewa kusikiliza kesi kwa wakati.

 "Tunatarajia Serikali zetu zitaona umuhimu wa Majaji wetu kuishi hapa nchini kuboresha utendaji kwa mwaka 2020 tumeamua kesi 50 ambazo hazijasikilizwa ni zaidi ya 100 na kila wiki tunapata kesi mpya kutoka popote ndani ya Nchi wanachama wanachi waitumie mahakama hii ni yak wasiogope,"alieleza Okubo.

 Aidha alieleza kwamba wamekuwa wakishirikiana na mawakili wa hapa nchini kuwapa elimu ya majukumu  yao kwa kuwapa mafunzo namna ya kuwasaidia wananchi kufanya maamuzi sahihi kulingana na  kesi zao ili kuoata haki.

 "Kama mawakili hawaelewi ni ngumu mwananchi kuelewa Sasa tunashirikina na Kitengo Cha Tanganyika Law Society (TLS)

ili walete mawakili wao tuwafunze namna ya kuwaelekeza wnanachi kuchambua kesi ipi isikilizwe na mahakama yetu au nyingine maana watu wanachanganya unakuta mtu anauliza mambo yanayosimamia na court ya AU au kuuliza kule masuala tunayofanya sisi,"alieleza Okubo.

 Ikumbukwe kuwa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, iliundwa mwaka 2006 ambapo  jukumu kubwa la mahakama hiyo ya haki ya EAC ni kuhakikisha  mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unafuatiliwa na kulinda utengamano katika ukanda huo ikunganishwa na Nchi sita za Burundi,Kenya,Rwanda,Sudani Kusini, Tanzania na Uganda.

 

 

 

Post a Comment

0 Comments