TAASISI ZA KISHERIA ZAOMBWA KUFUNGUA OFISI VIJIJINI.

 


📌STEPHEN NOEL.

TASISI za Masada kisheria na za kutetea Haki na zinazo toa msaada wa kisheria zimeobwa kufungua ofisini zao vijiji tofauti na sasa ambapo tasisi nyingi zimejikita mjini  na makao makuu ya wilaya. 

 Ombi hilo limetolewa na wanachuo wa chuo cha walimu Mpwapwa katika kuelekea kilele cha  wiki la sheria na miaka 100 ya kuanzishwa kwa mahakama kuu walipo kuwa wakiongea  chama cha majaji na mahakimu wanawake TAWJA( Tanzania Women Judges Association).waliofika chuoni hapo kutoa Elimu. 

 Bwana Athuman Lan'gu mwanachuo mwaka wa tatu amesema kuwa vyama vingi vinavyotoa misaada ya kisheria wamejikita kufungua ofisi mijini na makao makuu ya wilaya ambapo changamoto nyingi zinakuwa vijiji kutokana na uelewa mdogo wa masuala mtambuka ya maisha haki na maendeleo  yao. 

 Amedai kuwa  changamoto nyingi zinazo wakabili watu wa vijijini ni ukatili wa kijinsia, migogoro ya Ardhi ,ndoa na masuala ya kuhusiana na wosia na miradhi ambayo watu wengi hupoteza haki zao kutokana na kushidwa kuelewa changamoto zao zinatatuliwaje. 

 Naye Eisante Nassaly amesema kuwa pamoja na changamoto hizo pia jamii za vijijini  zinakabiliwa na changamoto nyingi za masuala ya haki ambayo Tasisi za utetezi ziweze kuwasaidia bila kujali mazingira waliopo. 

"Najua inaweza ikawa ngumu kulingana na mtaji lakini bora wangekuwa wanatoa huduma za mkoba za kutembelea vijiji walau Mala moja kwa miezi mitatu ili kuweza kuwasaidia watu wa vijijini "aliongea. 

 Kwa upande hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya Nurupedesia Nassary alikili kuwapo kwa tasisi chache za misaada ya kisheria vijijini kunakupelekea kuongezeka kwa vitendo vya ukatili wa kinjisia na vifo vitokanavyo na wivu wa mapenzi. 

 Amesema pamoja na kutokuwapo kwa tasisi hizo  wananchi wajenge moyo wakutembelea Mahakama na kujifunza au kuuliza masuala yanayo watatiza. 

 Katika kipindi hicho zaidi ya wanachuo 800 walufundishwa maada za ukatili wa kinjisia, Sheria ya Wosia na miradhi pamoja , sheria ya ndoa ,na mfumo wa mahakama. 

 Pia amedai wananchi waache kuziogopa mahakama wazitumie kujielimisha sheria ndogo ndogo zinazogusa maisha yao ya kila siku. 

 

Mwisho. 

 

Post a Comment

0 Comments