WAZIRI MHAGAMA AONYA MAAFISA KAZI WATAKAOFANYA UZEMBE KAZINI

 


📌DEVOTHA SONGORWA.

WAZIRI wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye ulemavu Jenista Mhagama amesema Serikali itawachukulia hatua za kisheria maafisa kazi watakaoshindwa kutatua migogoro inayojitokeza katika maeneo ya kazi.

Waziri Mhagama aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya  Mpango wa Mkakati wa Usimamizi wa Sheria za Kazi kuwajengea uwezo maafisa kazi 40  kutoka mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Morogoro,Singida,Geita, Njombe na Tanga yaliyoandaliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO).

Katika mafunzo hayo ambayo ni awamu ya kwanza ambapo watapatiwa mafunzo maafisa kazi 20 alisema ili kufikia azima ya serikali ya Tanzania ya viwanda ni lazima ufumbuzi wa changamoto katika maeneo ya kazi upatikane  ili wananchi kufanya kazi katika mazingira salama wakipatiwa haki zao za msingi akilitaka shirika hilo kuhusisha kundi la watu wenye uleamvu katika mafunzo yao.

“Niwasihi mtumie mafunzo haya  kama fursa ya kuleta mabadiliko acheni kufanya kazi kwa mazoea kuna migogoro mingi huko nje nisingependa msubiri yafike kwetu wakati nyinyi mpo ni wajibu wenu kutatua kero zao wapate stahiki zao mkumbuke wanategemewa na familia zao wanafanyishwa kazi bila mikataba , mishahara inachelewa wanaishi katika wakati mgumu hatutamfumbia macho atakayeleta uzembe katika hili,”alisema Waziri Mhagama.

Katika hatua nyingine aliagiza kutolewa ka taarifa ya robo ya mwaka kwa kila mkoa kuhusu utendaji wake hasa katika utatuzi wa migogoro maeneo ya kazi huku akipongeza mikoa iliyofanya vizuri katika kuchukua hatua za kutafuta suluhu ya masuala ya wafanyakazi.

“Kuna mikoa imefanya vizuri kushughulikia matatizo ya wafanyakazi kama Geita,Tanga,Iringa,Rukwa,Mtwara na Kilimanjaro niwaombe muongeze nguvu kwa Mbeya, Njombe,Dar es salaam,Morogo na Mra mmefanya vibaya taarifa zote ninazo sasa kupitia taarifa ya robo ya mnwaka kwa mkoa utakojirudia kufanya uzembe tutachukua hatua,”alieleza Waziri huyo.

 Aidha aliagiza kuanza kufanya kazi kwa mfumo wa kielektroniki wa utoaji wa vibali vya kazi kwa wageni kufikia Machi 20 mwaka huuu akiisitiza maafisa kazi wote nchibni kuendesha kliniki ya kazi kila ijumaa ya mwisho wa mwezi na kutoa taarifa ya utekelezaji wake.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO)Maridadi Fanuel alisema mafunzo hayo yamelenga katika maeneo mbalimbali ikiwemo ukuzaji wa ajira zenye staha,hifadhi ya jamii,majadiliano ya utatu kukuza uhusiano na haki katika sehemu za kazi.

“Mkurugenzi wetu anaishukuru Serikali kw aushiriakiano ambao imekuwa ikitupatia  ILO, tunashirikiana na wizara yenye dhamana  kuwajengea uwezo tunatamani kuona kukanuwa na uhusiano mzuri katia maeneo ya kazi, wafanyakazi watahaminiwe tuwe sehemu ya kutatua shida zao shirika hili lilianzishwa mwaka 1919 likilenga kutetea haki za kijamii katika eneo la kazi,”alifafanua Mwakilishi huyo.

Naye Naibu Waziri Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu weney ulemavu Ummy Nderiananga alisema ushirikishwaji wa kundi hilo utasaidia kuapata ajira na kuifanya jamii kutambua thamni yao akisema kuwa bado kuna changamoto ya uotaji wa ajira  katika sekta binafsi.

“Niliombe Shirika la ILO wakati mwingine kutoa mafunzo kw akundi la wawatu wenye ulamevu bado kuna shida katika Nyanja ya ajira sasa ikiwa tunataka kufikia katia malengo ya maendeleo endelevu ifikapo 2030  ni lazima tusimamie kundi hili kupata kazi za staha  na wasibaguliwe kutoaka na ulemavu wao wapewe fursa kama wengine ,”alieleza Waziri Ummy.

 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments