MCHAKATO WA KUTUNGWA KWA SHERIA YA TEHAMA KUANZA.

 


📌DEVOTHA SONGORWA.

 WIZARA ya  Mawasiliano na Teknolojia ya  Habari imeendelea na mchakato wa kujadili mapendekezo ya kutungwa kwa sheria ya Tehama.

Akizungumza  wakati wa kikao cha kujadili mapendekezo ya kuundwa kwa sheria ya Tehama, dokta Zainab Chaula amabaye ni Katibu mkuu wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya habari amesema kuundwa kwa sheria ya Tehama kutasaidia mambo mengi katika nyanja mbalimbali kiuchumi,kiusalama na maendeleo ya teknolojia.

Amesema Wizara imejipanga kufanya mambo makubwa kupitia uundwaji wa sheria ya Tehama ndiyo maana ya kuandaa kikao maalum leo na wadau ili kupata maoni mbalimbali ya uboreshaji wa miundombinu ya mawasiliano.

“Kuundwa kwa Wizara mpya ya Mawasiliano na Teknolojia ya habari lengo ni kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wake ikiwemo kuboresha vyombo vya mawasiliano vilivyo chini ya wizara kwa kuimarisha mifumo ya Tehama ’’ alisema Chaula.

Pia katibu alisema Tanzania ishafikia uchumi wa kati sasa kwa hiyo kupitia sheria ya Tehama ni mchakato wa kufika uchumi wa juu na pia ikumbukwe sheria hii ni ya muda mrefu kinachofanyika ni kuiboresha kwa michango kutoka kwa wadau.

Kwa upande wake Lugano Rweitaka Mkurugenzi wa kitengo cha sheria katika wizara ya mawasiliano na teknolojia ya habari alisema kwa sasa mambo mengi yanafanyika kwa msaada wa teknolojia ikiwemo biashara,mikutano na elimu hivyo basi Wizara kupitia vyombo vyake kama shirika la posta na kampuni ya mawasiliano ya simu (TCCL) vitakuwa mihili mhimu.

Hata hivyo kupitia mkongo wa taifa ni moja ya michakato ya uimarishaji wa teknolojia ya mawasiliano ili kusaidia kupanua wigo wa sekta hii ikiwa ni njia ya kupambana na mambo mbalimbali mtandaoni ikiwemo makosa ya kimtandao.

“Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) ni moja ya vyombo vilivyoboreshwa katika mfumo wa Tehama na utendaji wake ni ishara ya maendeleo ya teknolojia nchini kwa hiyo sheria ya Tehama na itakuwa na mchango mkubwa” amesema Rweitaka.

Mhadhili wa Chuo cha teknolojia ya habari Nkundwe Moses ni alisema uwepo wa wadau kutoka wizara mbalimbali serikalini na wataalamu kutoka vyuo vikuu ni ishara ya utekelezaji wa kujadili mapendekezo ya kutungwa kwa sheria ya Tehama itakayo kuwa na mashiko kwenye jamii.

“Lakini Tehama ni moja ya vitu mhimu sana duniani kwani licha ya kuwepo kwa ulinzi ,kuboreshwa kwa mifumo ya mawasiliano kutasaidia kuimarisha ulinzi mtandaoni kwani matumizi kuna mengine yapo kinyume na utaratibu” amesema Moses.

 

Post a Comment

0 Comments