📌 MWANDISHI WETU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan akitoa Heshima za Mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa
aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati
Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma
Akihutubia wakati wa shughuli ya kitaifa kuaga mwili wa
Magufuli kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Rais Samia ametoa hofu
wenye mashaka kuhusu uongozi wake akisema yuko tayari na anao uwezo mkubwa wa
kuliongoza taifa.
Rais Samia amesema licha ya yeye
kuwa ni mwanamke, yuko imara na kwamba amepita kwenye mikono ya hayati Magufuli
na hivyo amejifunza mengi kwa sababu alikuwa sio mtu wa kuyumbishwa na mwenye
msimamo thabiti kwa kile alichoamini kina maslahi kwa Watanzania na kwamba yeye
ataliongoza taifa bila mashaka yoyote.
Kwa wale ambao wana mashaka mwanamke huyu ataweza kuongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nataka niwambie huyu aliyesimama hapa ni rais, wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambaye maumbile yake ni mwanamke
Rais Samia Suluhus
Hassan
Aidha amesema yeye pamoja na
viongozi wenzake wako tayari kuiendeleza miradi yote iliyoanzishwa na serikali
chini ya uongozi wa Magufuli.
0 Comments