NDEJEMBI AIAGIZA TAKUKURU KUPAMBANA NA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI



📌RHODA SIMBA

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais  Menejimenti ya utumishi  na utawala bora Deogratius  Ndejembi  ameiagiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU)kuongeza nguvu kwenye kesi za ubakaji na mimba za utotoni  ambazo zimekuwa zikiminywa kwenye ngazi za chini na kusababishwa wahanga kukosa haki zao.

Ameyasema hayo leo  jijini hapa wakati akifungua mkutano mkuu  wa mwaka wa viongozi wa Taasisi  hiyo. 

 

Amesema hivi karibuni serikali imegundua kuwa kumekuwa na mtindo ambao sio mzuri kesi nyingi  zinazohusu rushwa ya ngono , ubakjaji, na mimba za utotoni  zimekuwa zikiharibika na kupoteza ushahidi.

“Serikali imejipanga kuhakikisha kesi zote zinazohusu rushwa ya ngono aendelezwa  na kama kuna mzazi  atabainika na kosa la kumaliza kesi hizo  atachukuliwa hatua kwasababu sheria ipo inayomtaka kila mzazi kutimiza wajibu wake,

“Nasisitiza kama kuna mzazi anafanya hivyo atambue kuwa anafanya kosa kisheria na wanakuwa wanalea kosa la rushwa ya ngono na ubakaji kuendelea kushamili katika jamii,”alisema



Ndejembi amewaagiza TAKUKURU katika mipango  mikakati yao ya mapambano ya rushwa kuelekeza  kwenye vyuo vyote nchini kuhakikisha wanamaliza suala la rushwa ya ngono ambako kwa kiasi kikubwa imeshamili.

Mmefanya vizuri kwenye utafiti mliofanya ndani ya vyuo vikuu viwili yaani UDOM na UDISM sasa ni wakati mwafaka nguvu zenu mkazielekeza kwenye vyuo vyote nchini kwani bado tatizo la rushwa ya ngono lipo hata huko

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TAKUKURU Brigedia Jenelali John Mbungo ametaja mipango mikakati ya miaka mitano ijayo kuwa ni kuhakikisha wanatekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi(CCM) ikiwa ni pamoja na kuboresha mfumo wa utendaji kazi.


Mkurugenzi wa TAKUKURU Brigedia Jenelali John Mbungo akitoa neno

Amesema katika awamu hii ya pili sasa ni wakati wa kutekeleza maagizo yanayotolewa na Rais Dk John Magufuli na kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake bila kuonewa.

“Tumejipanga katika awamu hii ya pili tutahakikisha tunamaliza tatizo la rushwa ya ngono ambalo kipindi cha nyuma ilikuwa imeshamili hasa katika taasisi za elimu na makazini, na kuhakikisha wananchi wanapata elimu  kuhusu kutoa na kupokea  rushwa,”alisema

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Bilinith Mahenge ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kusimamia na kuziba mianya ya rushwa kwenye nyanja  zote.

Ilikujenga nchi iliyoendelea lazima upambane na rushwa mabae ndio adui mkubwa wa maendeleo katika nchini nashuru serikali imejitaidi na inaendelea kujipanga kudhibiti


Kikao hicho kilichokutanisha watendaji wa TAKUKURU nchi nzima  kina lengo la kutatua changamoto zinazowakabili watendaji wa taasisi hiyo sambamba na kuweka mikakati ya mapambano ya rushwa  katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Post a Comment

0 Comments