SPIKA NDUGAI ALIVYOGUSWA NA KIFO CHA JPM,AZITAKA KAMATI KURUDI DODOMA



📌DEVOTHA SONGORWA


SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Job Ndugai ameeleza kusikitishwa na kifo cha Rais wa Awamu ya Tano,Dk.John Magufuli kilichotokea Machi 17 mwaka huu katika hospitali ya Mzena,Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Spika Ndugai ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Spika jijini Dodoma ambapo alisema Bunge limepata pigo kubwa kwani Rais MAGUFULI alikuwa miongoni mwa mihimili mitatu ya Nchi.

Pia Aliongeza kuwa Rais Magufuli katika uongozi wake alikuwa ni Rais mjenga Nchi hasa katika maeneo ya miundo mbinu ikiwemo barabara,sekta ya Afya na elimu.

Tumepokea kwa huzuni kubwa na majonzi hapa Bungeni mimi binafsi nilishindwa kulala baada ya kupokea taarifa za kifo chake usiku tunatoa pole kwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassani, Mjane mama Janeth Magufuli, familia nzima,Serikali na wananchi

Spika Ndugai.

Kufuatia kifo hicho Spika Ndugai amezitaka Kamati za Bunge zote na wabunge waliokuwa katika ziara za kukagua miradi ya mendeleo katika maeneo mbalimbali nchini kurejea haraka Dodoma.

Alieleza kwamba watanzania wanayo Kazi kubwa kuhakikisha wanendeleza ngwe aliyoiweka  na kushiriki kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 202-2025 na Kuendeleza Kazi zote alizozifanya kupitia hotuba alizozitoa hapa Bungeni yeye mwenyewe tunazisimamia KWA faida kubwa ya watanzania.

"Mwenyezi Mungu atutie nguvu sisi watanzania Rais Magufuli ameacha historia kubwa kwa  Taifa hilo Bwana alitoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe," amesema Spika Ndugai.

Post a Comment

0 Comments