TAIFA STARS KUIKABILI GUINEA NA MAJONZI

 


TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo inashuka inashuka katika uwanja wa Nuevo Estadio de Malabo nchini Guinea ya Ikweta kuwakabili wenyeji timu ya taifa ya nchi hiyo katika mechi ya kufa au kupona ya kusaka tiketi ya kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Afcon 2022.

Stars itashuka uwanjani ikiwa na majonzi kutokana na kuondokewa na Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli aliyefariki Machi 17, mwaka huu wakati kikosi hicho kikiwa kambini nchini Kenya kwaajili ya maandalizi ya mchezo huo.

Stars ina kumbukumbu nzuri dhidi ya Guinea ya Ikweta, ambapo katika mchezo wa awali iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Tanzania ipo Kundi J pamoja na Guinea ya Ikweta, Libya na Tunisia ambao ndio vinara wakiwa kileleni na pointi zao 10 wakifuatiwa na Guinea ya Ikweta yenye pointi sita, ikifuatiwa na Tanzania yenye pointi nne na Libya ipo mkiani ikiwa na alama tatu.

Tayari timu zote zimeshacheza michezo minne, hivyo kila timu imebakiwa na michezo miwili na Tanzania, Libya na Guinea ya Ikweta zinapigana kikumbo ili kupata nafasi ya kuungana na Tunisia ambayo tayari imefuzu.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen, Kocha Mkuu Kim Poulsen amesema wamefanya maandalizi mazuri kuikabili Guinea ya Ikweta na baadaye Libya japo ana amini haitakuwa kazi rahisi.

Kila mmoja nia yake ni kufanya vizuri ili kukata tiketi ya kucheza Afcon jambo ambalo ni matamanio ya kila mchezaji

 Poulsen .

 CHANZO:HABARI LEO

Post a Comment

0 Comments