VYAMA VYA USHIRIKA KOTE NCHINI VYATAKIWA KUANZISHA MIFUKO YA UTAFITI KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAKULIMA.

 

📌FAUSTINE GALAFONI.

Vyama vya Ushirika hapa nchini vimetakiwa kuanzisha mifuko ya utafiti hali itakayosaidia kutatua changamoto za wakulima kwa ufasaha.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Naibu katibu mkuu wizara ya kilimo Prof.Siza Tumbo wakati wa ufunguzi wa kongamano la kwanza la tafiti za ushirika ambalo limeandaliwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini[TCDC].

Prof.Tumbo amesema fedha za kutegemea wadau kutoka nje zimekuwa na masharti magumu hivyo ili kuondokana na vikwazo ni vyema kuanzisha mifuko ya utafiti.

“Tume ya Ushirika na vyama vikuu vya ushirika mkianzisha mifuko ya fedha za utafiti itasaidia sana ,maana fedha hizi za kutegemea wadau wan je ya nchi wanakuwa na masharti mara niandikie andiko kwa kiingereza ,muwasilishe kwa lugha ya kiingereza ,amesema.

Aidha,Prof.Tumbo amesema licha ya kuwezesha tafiti nyingi nchini,bado tafiti hizo  hazina majibu ya kero za wananchi hivyo kuwataka watafiti kutumia muda mwingi kufanya tafiti za masuala ya masoko huku pia akionya kwa baadhi ya wana Ushirika wanaoingia kwenye vyama hivyo kwa lengo la kujitajirisha  .

Naye Mrajisi wa vyama vya ushirika nchini Dkt.Benson Ndiege amesema  kuwa lengo la kongamano hilo ni fursa kwa kuwa limewakutanisha  wadau wa maendeleo ya ushirika kukutana na wanachama ,viongozi watendaji hivyo kuwa na matumaini zaidi katika kuleta matokeo ya tafiti mbalimbali za ushirika zilizowahi kufanyika na mapendekezo yake na kupata utatuzi wa changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

 Sambamba na lengo kuu,Mrajis huyo ameainisha  matarajio mengine kwenye kongamano hilo ni kupata mambo yatakayoibuliwa na washiriki ikiwa ni pamoja na vipaumbele vitakavyoainishwa vitafanyiwa utafiti ambapo maamuzi yake yatakuwa shirikishi ili kurahisisha utekelezaji.

Kwa upande wake   Meneja mkuu  chama cha ushirika cha mradi wa pamoja zao la tumbaku[TCJE]Bakari  Hussein amesema bado suala la elimu lipo chini kwa wana ushirika hivyo inahitajika zaidi na si kwa viongozi pekee

                                            ANGALIA PIA KWENYE CPC TV

                                                                     ðŸ‘‡ðŸ‘‡ðŸ‘‡

                                  


Post a Comment

0 Comments