YPC YAIPONGEZA SERIKALI KWA KUFANYA MABORESHO SERA YA VIJANA .

 




📌FAUSTINE GIMU  GALAFONI 

TAASISI  ya  shirikisho la Vijana viongozi nchini,Youth Partnership Countrywide [YPC] imeipongeza Serikali kwa kuendelea kufanyia maboresho sera ya vijana ikiwemo Sera ya vijana  ya namna ya kupata mikopo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika kongamano la vijana viongozi jijini Dodoma,Mkurugenzi mtendaji wa  Taasisi ya vijana ya (YPC) Israel Irunde amesema  sera  ya vijana kwa sasa inaruhusu kukopesha kuanzia vijana watano na si kumi kama ilivyokuwa awali .

"Tangu mwaka juzi na Mwaka jana tulizungumza sana kuwasaidia vijana  kwanini  vijana wapewe mikopo wakiwa  10   wakati hawafahamiani ,kwanini watu  wenye ulemavu walazimishwe kukaa kwenye kikundi cha watu 10 wakati ni vigumu kuwakutanisha hata wawili lakini hivi karibuni Waziri Jafo wa TAMISEMI tayari alishatangaza kanuni zilishabadilishwa sasa vijana wanaweza kupata mikopo hata wakiwa watano na watu wenye ulemavu anaweza kupata mikopo serikalini hata akiwa mmoja"amesema.

Aidha,Mkurungenzi huyo wa YPC amesema  ni wajibu  kuwathamini  vijana  pamoja na kuwepo wa maboresho ya sheria ya mahusiano kazini .

"Mara nyingi sana tumepigania kuhakikisha vijana wanapata kazi zenye staha wakiwa wanaajiriwa au wamejiajiri wenyewe ,vijana wasitumiwe kama ndala ,wajisikie nao wana maisha ya baadaye kuliko kukaa tu kwenye kazi ya kukupatia chakula wakati mwingine chakula nacho shida ,ili kila mmoja atoke kutoka kwenye eneo alilokuwa nalo hivyo hapa pana hitaji maboresho zaidi sheria ya mahusiano kazini "amesema.




Fred Mtei  ni Mratibu  wa shiriki wa Kongamano la YPC amebainisha lengo la kongamano hilo ni pamoja na namna ya kutatua changamoto za vijana huku Irine Ringo akisema  moja ya manufaa ya kongamano hilo ni kujiamini kwa vijana .

Mwasilishaji wa Mada mbalimbali katika kongamano hilo la vijana la YPC, Adv.Dominick Nduguru  mkurugenzi kutoka Taasisi ya Maendeleo ya vijana ya Open Mind Tanzania amesema kuna uhitaji wa sera bora ya vijana pamoja na watu wenye ulemavu kuhusishwa zaidi juu ya mapitio ya sera ya vijana.

 Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kazi,Vijana ,ajira na wenye ulemavu  Amina Sanga ametoa wito kwa vijana kuendelea kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali kwa vijana ikiwemo mafunzo ya kujitolea ya kuwajengea uwezo namna nzuri ya kuchangamana na watu mbalimbali ili kupata fursa zinazoweza kujitokeza ikiwemo kubadilishana ujuzi na uzoefu.


"Vijana tunapaswa tuamke,tena ukisikia kuna warsha sehemu fulani changamkia ,changamoto ya vijana wa kileo akisikia kuna semina sehemu fulani ya kumjengea uwezo lazima atauliza kuna posho,hajui kuna sehemu nyingine semina za kujengewa uwezo mpaka ulipie lakini Tanzania tuna bahati nzuri sana unapewa ujuzi lakini unataka ulipwe na ukisikia hakuna posho hauhudhurii,kumbuka unapochangamana na watu mbalimbali hiyo ndiyo fursa na mwanzo wa  maisha yako hata siku moja wanaweza kukutafuta kuwa yule kijana ana mchango mzuri sana tumchukue tu  huyo"amesema.

Taasisi ya shirikisho la vijana ya YPC  ilisajiliwa mwaka 2003 kama kampuni isiyopata faida chini ya sharia ya makampuni  na mwaka 2019 ilisajiriwa kama asasi ya Kiraia[NGO]ikiwa na lengo wa kujenga uwezo kwa vijana jinsia zote  ambapo katika kongamano hilo vijana kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wamekutana kujengewa uwezo ikiwa ni pamoja na namna  ya vijana kufikia fursa .

 

Post a Comment

0 Comments