MFUMO DUME, UMASIKINI NA IMANI ZA KISHIRIKIANA NDIO CHANZO CHA VITENDO VYA UKATILI

 




📌HAMIDA RAMADHANI

IMEELEZWA Kuwa Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto wa kike Unabebwa na dhana kubwa ya Mfumo dume Umasikini na imani za kishirikiana.

Katika kuhakikisha wanapunguza na kuondoa kabisa vitendo hivyo vya ukatili Taasisi  ya TGNP Mtandao imekuwa ikijihusisha na Harakati za ukombozi wa wanawake Kimapinduzi nchini Tanzanian ,Barani Afrika na kwengineko Duniani.

Taasisi hiyo ya TGNP Mtandao jana April  14  imetoa mafunzo kwa baadhi ya wabunge wanawake lengo likiwa nikuwepo  kwa elimu juu ya vitendo Vya ukatili vinavyofanyika lila siku katika jamii ili nawao waende wakapaze sauti zao Bungeni hasa kipindi hiki cha vikao vya Bunge la Bajeti vinavyoendelea.

Jackline Ngoyani msongozi ni  Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Ruvuma ambaye ni moja Kati ya wabunge wanawake walioshiriki  mafunzo ya shirika la (TGNP) Mtandao juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Amesema kupitia mafunzo hayo Wamepata uelewa mpana ambapo sasa, wanakwenda kuishauri serikali kuweka Mpango Mkakati utakaoenda mpaka katika jamii inayoishi na wanawake na watoto iliwaweze kuondokana na kutokomeza kabisa ukatili.

Naye Mbunge Viti Maalumu kupitia tiketi ya Chama cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ester Matiko amesema kupitia mafunzo hayo Wameweza kupata elimu na kujua zaidi takwimu za Mikoa  inayoongoza kwa ukatili wa kijinsia.

Sasa tumeweza kutambua serikali inatakiwa kutenga bajeti ya kutosha katika kuhakikisha mapambano dhidi ya ukatili kwa wanawake na watoto yanaendelea.

Matiko.

Kwa Upande Wake  Mwasi Damas  Mbunge wa Viti Maalum na ni mwakilishi wa Vijana Taifa kutoka  Mkoa wa Mwanza amesema  wamepewa mafunzo ya ukatili kwa wanawake na watoto lengo likiwa ni kuhakakisha wanapata uelewa juu ya vitendo Vya ukatili kitakwimu hasa kipindi hiki cha Bunge la bajeti.

" Tumeweza kubaini ni Mazingira gani ya ukatili yanatokea na na mazingira gani yamekithiri na hatua kama  nchi, serikali na Asasi za kiraia zimechukua kupunguza tatizo hili,".

Na kuongeza kuwa"Mafunzo Haya yamekuja kwa kipindi Muafaka kwani wakifika bungeni tutaisemea agenda hii kwa upanda wake ili fedha itengwe kulingana na upande wa tatizo hili,"amesema Mwasi.

Aidha ametoa wito kwa wanaharakati wakupinga ukatili na wabunge wote watumie nguvu kubwa kulisemea jambo hilo bila kuwasahau Vijana wakike kwani ndio wameonekana wahanga wakubwa wa tatizo hili.

 

Post a Comment

0 Comments