MKUTANO WA MAWAZIRI WA NCHI ZINAZOZALISHA MADINI KUFANYIKA KWA NJIA YA VIDEO

 


📌FAUSTINE GIMU GALAFONI

MKUTANO wa saba wa Mawaziri wa nchi za Afrika zinazozalisha madini ya Almasi  umefanyika leo   huku ukitaraijiwa kuhitimishwa kesho kwa njia ya video ambao utahusisha ushiriki wa Mawaziri wa nchi wanachama na wataalamu wa madini kutoka nchi 12.

 

Hayo yamebainishwa leo Jijini  Dodoma na Waziri wa Madini Dotto Biteko wakati akizungumza  na Waandishi wa Habari ambapo amesema lengo la Mkutano huo ambao ni wa siku mbili ni kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta hiyo.

Akifafanua zaidi Biteko amesema,Tanzania  ni nchi mwenyeji wa Mkutano huo na kwamba itapokea Uenyekiti wa jumuiya hiyo kutoka nchi ya Jamhuri ya Namibia ambayo inamaliza muda wake wa kipindi cha mwaka mmoja.

Waziri Biteko amefafanua kuhusu malengo ya Jumuiya hiyo ambapo amesema ni pamoja na kuzipatia nchi zinazozalisha Almasi Afrika jukwaa la kuzikutanisha nchi zoteza Afrika ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu.


Jumuiya hiyo ilianzishwa kwa mujibu wa Azimio la Luanda, Angola na sheria za  nchi za Afrika zinazozalisha madini ya Almasi  mnamo mwezi Novemba ,2006 huku ikihusisha nchi 19 ambapo 12 kati ya hizo ni wanachama ,nchi saba ni waangalizi.

 

 

Post a Comment

0 Comments