RC MAHENGE AITAKA DUWASA KUKABILIANA NA WEZI WA MAJI

 


📌MWANDISHI WETU

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Dodoma (DUWASA) kukabiliana na wezi wa maji huku wakiwachukulia hatua watumishi wa mamlaka hiyo wanaochangia hasara kwa kutokuwa waaminifu.

Akizungumza mapema leo katika semina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa Jijini Dodoma Dkt.Mahenge amesama kuwa baadhi ya watumishi wa Mamlaka hiyo sio waaminifu na wanaingiza hasara ya mapato kwa kushirikiana na wananchi hivyo ni vyema wakawachukulia hatua ili kudhibiti wezi wa maji.

Tuhakikishe kuwa tunakabiliana na wezi wa maji na waharibifu wa miundombinu,wale wanaoiba vizibo na mifunuko ya maji taka kwa kuwa sheria zipo wakamatwe na wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria na kanuni zake,simamieni na wale ambao siyo waminifu wanao ''kula dili'' na wananchi za kuhusu kutumia maji bila malipo wakamatwe waondolewe kwenye utumishi wa DUWASA maana hao hawafai 

RC Mahenge.

Katika hatua nyingine Dkt Mahenge  ameipongeza Duwasa kwa jitihada kubwa inayofanya kuhakikisha inakabiliana na changamoto ya upatikanaji wa maji kwani hadi sasa jiji la Dodoma linaupugufu wa maji zaidi ya lita million 37 kufuatia kuzalisha lita Milion 103.

“Niwapongeze sana DUWASA kwa kuzalisha lita million 66 wakati kabla Serikali haijamia Dodoma tulikuwa tunazalisha lita million 61.5 kwa hiyo lipo ongezeko kubwa,niwapongeze kwa kuongeza uzalishaji wa maji na maji tunayozalisha sasa lazma tuyatunze na tuyalinde” Aliongeza RC Mahenge.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa bodi ya DUWASA,Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Neema Majule amesema maji ni kapaumbele na DUWASA imefanya kazi kubwa kukidhi mahitaji ya maji kutokana na ongezeko la watu Dodoma.

Duwasa imefanya kazi kubwa sana kipindi hiki ili kuweza kukidhi mahitaji ya maji na kukidhi ongezeko la watu Dodoma,Mtakubaliana na mimi kwa sasa kuna unafuu mkubwa sana hata kama kuna upungufu wa maji na hata kama kuna mgao wa maji lakini kwa kiasi kikubwa sana maji yameweza kutosheleza kwa jiji la Dodoma

Majule.

Naye Mbunge wa Dodoma Mjini Mh Antony Mavunde amebainisha kuwa Kuanzia mwezi wa kumi na moja hadi sasa visima 10 vya maji vimechimbwa kati ya visima 20.

“Na mimi kama mbunge kwenye jimbo hili naunga mkono jitihada za DUWASA kwenye kutatua changamoto hasa katika maeneo yaliyo pembezoni mpaka hivi sasa toka mwezi wa kumi na moja mwaka jana tumeshachimba visima kumi kati ya visima 20 nilivyoviahidi wakati wa kampeni na ninaamini vingine tutavikamilisha kwa wakati” Amesema Mavunde.

Aidha kukamilika kwa miradi miwili ya maji jijini Dodoma Mradi wa Farkwa na ule wa Ziwa Victoria inatajwa kuwa itasaidia kwa kiasikikubwa kuondoa adha ya upatikanaji wa maji kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments