SHIBUDA ATOA TATHMINI YA SERIKALI YA RAIS SAMIA

 



📌FAUSTINE GIMU GALAFONI

MWENYEKITI wa baraza la  Vyama vya Siasa Tanzania John Shibuna amemuomba Rais wa   Tanzania  Samia Suluhu Hassan akutane na vyama vya siasa ili waweze kupata nasaha zake.

 Shibuda ameyasema hayo   jijini  Dodoma  wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tafakuri maalumu ya kuhitimisha kipindi cha maombolezo cha aliyekuwa Rais wa Serikali ya awamu ya Tano Hayati Dk John Magufuli.

Shibuda ambaye pia  ni mbunge mstaafu jimbo la Maswa Magharibi mkoani Simiyu amesema hotuba ya kwanza ya Rais Samia ilionesha  maono na fikra sahihi  za wadau wa tasnia ya siasa na imethibitisha mitazamo ya kusimamiana kati ya serikali na wadau wa siasa.

Naomba fursa hii kuomba siku ikikupendeza Rais Samia Suluhu Hassan utuite viongozi wa baraza la vyama vya siasa Tanzania tuje kupokea nasaha zako 

“Kwa kipindi kifupi ulichoongoza umeonyesha kuwa wewe ni kiongozi bora na mbobezi kwa ujenzi na ufumbuzi kwa kuunda makutano kati ya fikra za wadau wa vyama vingi na umaana wa hekima ya ujumbe wa hotuba yako ya machi 19 mwaka huu,”alisema

 Shibuda amesema  Baraza la vyama vya siasa linampongeza Rais Samia kwa kuwarejeshea matumaini ya  watanzania .

Naipongeza serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza pale alipoishia Hayati Dk Magufuli huo ni uamsho mpya  unaokweza morali na kukuza hali mpya kwa umma kuwa  rafiki na serikali,

 Shibuda amesema  Hayati Rais Dk Magufuli ameacha dhana kwenye vichwa vya watanzania vya kujitegemea kiuchumi  na ndoto huru ya maendeleo na ustawi wa jamii,uchumi na taifa.

Amesema hayati DK Magufuli ameondoka duniani akiwa amedhibiti dhana potofu na ovu ya nchi kujengwa na wenye moyo na klul;iwa na wenye meno hususani wenye mirija ya unyanyasaji wa mali na rasilimali za taifa kupitia watu wa ndani na nje ya nchi.

“Hayati Dk Magufuli katuachia utumishi wa fikra zilizopigwa msasa na kaacha masomo ya maangalizo na maono ya hekima ya kuongoza taifa letu ,

“Hayati Dk Magufuli amemaliza wajibu wake hapa duniani ameiacha serikali na wananchi hivyo tuwe na misimamo thabiti ya kukataa vishawishi vya chui waliovaa ngozi za kondoo wenye nia ovu na katili ya kudhuru na kudhurumu maisha ya furaha na heshima za utu na uhai wa binadamu wa Tanzania,”alieleza

Mwenyekiti huyo wa  baraza la vyama vya saiasa  ametoa usahuri kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba kuibua uvumbuzi wa kisheria wa kusadikisha dhamila njema ya serikali kulinda maslai ya kati ya benki na mteja anayeweka pesa zake.

Amesema kodi na VAT zinadhoofisha uchangamfu na ustawi wa biashara hivyo wizara ya kilimo na wizara ya uwekezaji na wizara ya fedha kuwa na makutano mara kwa mara  kuunda sheria madhubuti zatakazo changia kukuza sekta muhimu ya biashara hapa nchini ambayo itachangia kuongeza wigo wa ukusanyaji kodi

 

 

Post a Comment

0 Comments