TGNP YASAIDIA WANAWAKE KUJITAMBUA,KUJUA HAKI ZAO NA KUTETEA

 


📌HAMIDA RAMADHANI

MRATIBU wa Mtandao wa jinsia Tanzania ,Tanzania Gender Networking Programme (TGNP) Zainabu Mmari amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa harakati za ukombozi wa wanawake nchini  Wanawake wengi wameweza kujitambua,kujua haki zao na kutetea mahitaji yao ya Msingi katika ngazi husikia.

Akiongea na waandishi wa habari Jijini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa mafunzo waliopatiwa wabunge wanawake juu ya masuala mazima yanayohusu ukatili Zainabu amesema  wao kama TGNP muda wa miaka mitano nyuma wameamua kuwekeza nguvu kubwa katika ngazi ya Jamii.

Sio kwamba tumeacha kujikita katika ngazi ya serikali Kuu hapana tumeamua kufanya hivyo ili tuweze kuwafikia wananchi wengi ambao ndio wameonekana ndio wenye uhitaji.

Zainabu Mmari.

Amesema kuwa wamefanya kazi katika maeneo ya upatikanaji wa kijamii ikiwemo Afya, Elimu Maji na  sasa wamejikita katika eneo la Kilimo ambapo ndipo kumeonekana kunakundi kubwa la wanawake wengi zaidi ya  asilimia 55 wamejiajiri kwa kutumia Kilimo. 

Pia amesema wameanza kuangazi  kwa wanawake ambao ni wachimbaji wadogo wadogo na kuna maeneo ambayo wanafanyia kazi kama vile Wilaya ya Morogoro vijijini ,Wilaya ya Mbeya Vijijini,Wilaya ya Shinyanga Kishapu,Tarime na Kasulu.

Amesema wameweza kujenga nguvu kubwa ndani ya jamii katika kumkomboa mwanamke kimapinduzi na kuaanzisha vituo  vya taarifa na maarifa  ambavyo vinaendeshwa na wanawake waliowezeshwa na  wanaotambua haki zao,wanaotetea masuala ya kijinsia,wanauwezo wa kufuatilia ngazi tofauti tofauti za Serikali kuanzia ngazi ya kijiji ,Kata,hadi Halmashauri na kuona ni namna gani masuala hayo yanaweza kuingizwa kwenye Mipango na bajeti za Serikali.

Kwa Kiasi kikubwa tumefanikiwa mpaka kufikia kwa baadhi ya Halmashauri wanapokuwa na vikao vyao vya kupitisha bajeti wanatualika hivyo vituo vya Taarifa na Maarifa ngazi ya Jamii kwa ajili ya kuangalia na kutoa mapendekezo yao ili yaweze kuingizwa kwenye bajeti za Halmashauri.

Zainabu Mmari.

ATHARI ZA VITENDO VYA UKATILI KWA WAWAKE NA WATOTO.

Amesema changamoto ni kubwa  kwani mwanamke au mtoto wa kike au mtu yoyote katika jamii anapofanyiwa vitendo Vya ukatili kwanza kabisa vinamuondolea kujiamini hata maendeleo yake hata ushiriki kwenye jamii unapungua.

" Na imeonekana wanawake wengi au watoto wa kike wanaofanyiwa ukatili kwasabau ya ukosefu wa kipato au uchumi mdogo kuanzia ngazi ya Jamii, familia na wakati mwingine anaweza kuona viashiria vya ukatili lakini anashindwa kuondoka kwasabau ya hofu ya kujifunza mwenyewe na familia kwa Jumla.

Amesema vitendo hivyo vimewaathiri Sana kwani utakuta mwanamke anafikia hatua ya kijifungia ndani kwasabau ya kunyooshewa vidole na Jamii vitendo hivyo vinawaharibu wanawake kisaikolojia.

Naye Mussa Jonasi ambaye anafanyia kazi na Shirika la TGNP  Mkoani Shinyanga Amesema mfumo dume Umasikini na imani za kishirikiana,mila kandamizi ndio chanzo cha vitendo Vya ukatili katika ngazi ya jamii hadi ngazi ya familia.

 

Post a Comment

0 Comments