USHAMIRI WA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI DODOMA BADO JUU.

 


📌FAUSTINE GIMU GALAFONI

HAYO yamebainishwa leo April 29,2021 jijini Dodoma na Naibu Waziri  wa Nchi,Ofisi ya Waziri mkuu,Sera,Uratibu,Bunge ,Kazi ,Ajira , vijana Patrobas Katambi katika ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa wadau wanaotekeleza miradi ya wasichana balehe na wanawake vijana .

Naibu waziri Katambi amesema   utafiti wa  mwaka 2016/17 umeonesha kuwa kiwango cha ushamiri kimeendelea kupungua sambamba na kiwango cha maambukizi mapya na vifo vitokanavyo na UKIMWI, Wastani wa Kitaifa ushamiri wa VVU ni wa asilimia 4.7,Mikoa yenye ushamiri wa juu ni Njombe (11.4%) na Iringa 11.3 na Mbeya (9.3%) ambapo ushamiri katika Mkoa wa Dodoma umeongezeka kutoka asilimia 2.9 hadi asilimia 5.

Mhe.Katambi amefafanua kuwa Katika utafiti huo watu 72,000  wanapata maambukizi mapya kwa mwaka na kati yao 40% ni vijana; kati ya hao vijana 80% ni wasichana wa umri wa miaka 15 – 24 ikimaanisha  kuwa kila kundi la vijana kumi wenye maambukizi 8 kati yao ni vijana wa kike na 2 ni vijana wa kiume.

Ni muhimu kuhimiza vijana na watu wote kupima ili kujua hali zao, kutumia dawa kwa waliogundulika  na VVU na kuepuka maambukizi ikiwa bado hawajapata maambukizi.

Katambi

 Aidha, Katambi amesema  kupitia matokeo ya utafiti wa 2016/17 Serikali iliona umuhimu wa kufanya jitahada za pamoja na wadau katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI, hususan katika kundi la vijana wa kike.  

 Katambi amesema malengo ya nchi ni  kufikia sifuri ya maambukizi mapya ya VVU, sifuri ya ubaguzi na unyanyapaa utokaonao na UKIMWI na sifuri ya vifo vitokanavyo na UKIMWI ifikapo 2030.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS),Dk.Leonard Maboko amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kuwaleta wadau na kuona wamefikia wapi na wamekutana na changamoto zipi pamoja na kuzitatua.

"Sisi TACAIDS kazi yetu ni kuratibu na ndio maana hapa kuna taasisi kazi yetu kubwa ya hili kundi ni kuratibu kila mwaka hivyo hichi kikao ni cha kuwaleta hawa wadau kuona wamefikia wapi na wamekutana na changamoto zipi pamoja na kuzitatua,ili kujadiliana tulipotoka tulipo na tunapoelekea,"amesema Maboko.

Dkt.Maboko amesema kuwa  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa aliagiza Tacaids ifanye kazi na vijana ambapo alidai kwa sasa wanafanya kazi nao hususan wasanii.

Hata hivyo Dkt.Maboko amesema kuwa takwimu zinaonesha vijana ni kundi lenye Changamoto katika maambukizi ya Ukimwi.

"Maambukizi mapya asilimia 40 yalikuwa yanatokea kwa vijana lakini asilimia 80 ya hao vijana ni wa kike,kwa umaalumu kabisa ndio maana hili kundi likapewa msisitizo huu.Takwimu zilituonesha hivyo tukaona kuna haja ya kuweka mkazo katika hili,"amesema

UMEISOMA HII?👇👇👇

DKT. NDUGULILE AFUNGUA MKUTANO WA 41 WA SATA WA NCHI ZA SADC

Post a Comment

0 Comments