UWT WAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA SULUHU HASSAN/WAPONGEZA TEUZI ZAKE.

 


📌DEVOTHA SONGORWA.

 JUMUIA ya Wanawake Tanzania ( UWT) imeahidi kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa majukumu yake kwa ajili ya manufaa ya watanzania.

 Akizungumza na waandishi wa habari ili kutoa tamko la Jumuia,Mwenyekiti wa UWT Taifa,Gaudensia Kabaka alisema  Chama kinamuamini kwani aliyoonyesha uwezo wake wa uongozi akiwa nafasi ya Makamu wa Rais.

Amesema UWT inampongeza kwa kuapishwa  kuwa Rais wa Tanzania mwanamke licha ya kupata nafasi hiyo katika hali ya majonzi kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Magufuli.

Amesema anaamini nchi iko salama chini ya uongozi wake kwani amekuwa na uwezo mkubwa wa kiutawala na uongozi hata wakati akiwa nafasi ya Makamu wa Rais hivyo watanzania wamuamini na kumpa ushirikiano wa kutosha ili nchi iweze kusonga mbele.

 "Tulipokea kwa masikitiko na simamzi kubwa taarifa za kifo cha Rais wetu hatujawahi kupata msiba wa kiongozi mkubwa hivyo akiwa madarakani tunatoa pole kwa watanzania wote,"alisema.

 Pia Mwenyekiti huyo alieleza kwamba UWT inaungana Serikali KWA ujumla chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika muendelezo wa siku 21 za maombolezo huku ikitoa pole kwa Rais Samia kwa msiba huo mkubwa kwa Taifa.

 "Tunaendelea kuwa pamoja naye tunapoendelea katika siku 21 za maombolezo ya msiba huu mzito kwetu na tunampongeza kwa utulivu aliuonyesha wakati wote wa msiba maana sisi watanzania tulikuwa tunamwangalia yeye lakini alikuwa mtulivu Sana hali iliyotufanya nasi watanzania kuungana pamoja," alieleza Gaudensia.

Hata hivyo amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mwanachama hai ndani ya Chama hatua iliyoonyesha mfano huku UWT ikijipngeza kwa kutoa Rais mwanamke hatari inayotoa chachu kwa kina mama kuthubutu kushika nafasi za uongozi. 

 Akizungumzia mwenendo wa utendaji wake akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alieleza kwamba ameanza vizuri kwa kumteua Dk.Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais pamoja na viongozi wengine wakiwemo Mawaziri na Manaibu Waziri.

" Sisi kina mama na watanzania wote tunakubaliana naye kuwa Makamu wa Rais anaendelea akamteua Balozi Hussein Othuman kuwa Katibu Mkuu Kiongozi kwakweli ameanza vizuri tunaamini watafanya Kazi vizuri kuwatumikia wananchi," alibainisha. 

 Kuhusu upande wa Afrika Mashariki alibainisha kwamba Tanzania ilikuwa nchi ya pili kuwa na Makamu wa Rais mwanamke ikifuatia nchi ya Uganda lakini kulingana na Katiba ya Tanzania mama Samia Suluhu Hassani anakuwa Rais kamili ikilinganisha na Katiba za baadhi ya nchi zingine ambavyo angekaimu nafasi hiyo kwa muda.

 "Kwa kweli Rais Samia ana sifa zote za kuwa Rais licha ya taratibu za Katiba kwamba Rais akifariki Makamu ndiye anachukua nafasi bado ana sifa za kuwa Rais na kufuatia uongozi wake kama Makamu alimsaidia Hayati Rais.Dk.Magufuli,"alieleza. 

 Aidha alifafanua kwamba uamuzi wa kutoa nafasi  kubwa za uongozi kwa wanawake katika Baraza la Mawaziri umeongeza idadi yao hali inayoendelea kutoa hamasa kwa wanawake kujituma na kuonyesha uwezo wao.

 "Zipo Wizara ambazo tunaamini zinawagusa wananchi moja zaidi ipo Wizara ya Afya, Wizara ya elimu,Wizara ya mambo ya nje,Wizara ya TAMISEMI , Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Watu wenye ulemavu na Wizara ya Maji tuna Naibu Waziri mwanamke anaamini watachapa Kazi,"alisema.

 Alihitimisha kwa kuwasihi viongozi wote walioteuliwa au kuendelea na nafasi zao kuviishi viapo vyao kwa kuwatumikia wananchi na kutokuwa wabadhirifu wa mali za umma,kulinda Katiba na kutekeleza miradi iliyoanishwa kwa mujibu wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pmaoaja na watanzania wote kukupa kodi kwa Maendeleo ya Taifa kama sehemu ya kumuenzi Hayati Rais Dk. John Magufuli. 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments