WATAALAMU ZAO LA PAMBA WATAKIWA KUSAIDIA WAKULIMA KULIMA KILIMO CHENYE TIJA



 ðŸ“ŒHAMIDA RAMADHANI

WAZIRI wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda amewataka wataalamu wa zao la Pamba kuwasaidia wakulima waweze kulima Kilimo chenye tija katika zao hilo.

Akizungumza leo jijini hapa katika kikao cha awali cha Bodi ya Pamba amesema  Wizara hiyo ipo mbioni kuanzisha Mfuko wa Utafiti ambao utawasaidia wakulima kulima Kilimo chenye tija.

Amesema zao la Pamba, limekua na changamoto ya kupanda na kushuka ambapo tatizo kubwa limeonekana  ni ukosefu wa pembejeo huduma za ugani hali ya hewa,na utulivu wa Soko.

Pembejeo na huduma za ugani zimekua  zikiendeshwa kwa sera,ambazo tumezitunga Sisi,sasa ni lazima tuweke sera nzuri ambazo zitamsaidia mkulima kulima kilimo chenye tija

Profesa Mkenda

Amesema Pamba ni zao muhimu kiuchumi na kisiasa na limekua likigusa Watu wengi nchini hivyo hatuna budi kuwekea mkazo ili wakulima waweze kulima mazao yenye tija.

Aidha amesema kwa mwaka 2021  Tanzania inatarajia kupata tani takribani laki nne ambapo ni tofauti na miaka ya nyuma.

Mwaka huu wa Kilimo ni tofauti na miaka ya nyuma ambapo tunatarajia kupata tani  laki 393,460  kwa miaka kumi hatujawahi kufikia tutakuwa na msimu mzuri

Mkenda

Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba  Marco Mtunga ameiomba serikali kutengeneza mfumo  utakaoweza kuwapatia maafisa ugani pikipiki na kujaziwa Mafuta  ili maafisa ugani waweze kupita kwenye mashamba ya wakulima kukagua na kubaini athari mapema za wadudu wekundu.

"Tunaomba hata hizi pikipiki za maafisa ugani zifungwe GPS ili afisa ugani aweze kutambulika anafanyia shughuli gani,na ni kwa wakati gani " amesema  Mtunga

Hata hivyo ameiomba serikali kumaliza deni la Shilingi billion 87,na  ambapo amesema endapo madeni hayo yatatatuliwa zao la pamba litasonga mbele. 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments