📌DOTTO KWILASA
KUFUATIA kukua kwa teknojia ya Mawasiliano nchini,Benki ya
CRDB inaendelea kufanya maboresho ya huduma zake ili kukidhi mahitaji ya Wateja
wao kulingana na wakati.
Moja Kati ya huduma hizo ni kuwawezesha wananchi
kufungua akaunti ya benki hiyo kwa kutumia simu ya kiganjani
popote alipo na kuepusha usumbufu.
Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Meneja
Mafunzo na Maendeleo ya Benki hiyo Edith Mwiyombela wakati akizungumza na
waandishi wa habari kwenye maonyesho ya pili ya elimu na Ufundi mabayi
yaliyoandaliwa na Baraza la elimu Tanzania(NACTE) yanaendelea katikaViwanja vya
Jamhuri.
Akiongea katika maonyesho hayo alisema hivi sasa
wamefanya maboresho katika huduma za kifedha na kuwa rahisi ikiwa ni pamoja na
kupunguza masharti kwa wateja .
Alisema,huduma hiyo itaondoa vikwazo ambavyo wateja
wengi huona kama kero kwao ikiwepo barua ya wadhamini ,barua ya Mtendaji,picha
ya paspoti pamoja fedha ya papo kwa papo ambapo kwa sasa unaweza kufungua
akaunti kisha ukahamisha fedha kutoka kwenye mitandao ya siku kwenda kwenye
akaunti.
Huduma hii imerahisisha sana,kwanza mteja atakuwa ameokoa muda ,wateja wengine walikuwa wanatamani sana kufungua akaunti lakini walikosa muda,wakati mwingine walitumia muda mwingi katika kutimiza vigezo au kukosa kabisa
Kwa upande wake Simon Mukajanga ambaye ni mshirika wa
programu ya uzamili katika benki hiyo alieleza vigezo na masharti vya
kufanikisha kujiunga na huduma hiyo ya kufungua Akaunti kwa kutumia
simu ya mkononi bila kufika Ofisi za Benki ambapo alisema mteja atatakiwa
kujisajili kwa kutumia namba ya kitambulisho cha uraia(NIDA).
Pamoja na hayo alifafanua kuwa huduma hiyo ina faida kwa
kuwa inatoa risiti kwa njia ya simu ili kumrahisishia mteja kuwa na kumbukumbu
ya miamala aliyoifanya na kuifanyia mipango katika maendeleo yake.
“Risiti inasaidia mtu kupangilia mipango yake katika
matumizi,tunawashauri wananchi kuitumia huduma hii kwani inaokoa muda kwa kuwa
huhitaji kusafiri ,utatumia simu yake huku akiendelea na mambo mengine ya
uzalishaji,”alisistiza.
0 Comments