IGP SIRRO ATANGAZA KUANZA KWA OPERESHENI MAALUM KUSAKA WAHALIFU

 


📌MWANDISHI WETU

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, ameutaja mkoa wa Kipolisi wa  Kinondoni kama kinara wa uhalifu nchini ambapo matukio ya uporaji, uvunjaji wa kutumia nguvu na uporaji kwa kutumia pikipiki yakiwa yameongezeka huku uhalifu mwingine mkubwa wa kutumia silaha za moto ukiwa umeshuka.

IGP Sirro amesema hayo jijini Dar es salaam, wakati akizungumza na Wenyekiti wa Serikali za Mitaa, watendaji Kata, pamoja na watendaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi ambapo amewataka watendaji wote kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha usalama unaendelea kuimarishwa.

Aidha, IGP Sirro ametoa muda wa wiki moja kuhakikisha wanakomesha vitendo vya kihalifu kwa kushirikiana na watendaji wengine huku akitoa wito kwa mgambo kuacha kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa.

Watendaji wa Kata na Wenyeviti wa Mtaa wanajukumu la kuhakikisha Ulinzi na Usalama katika maeneo yao unaimarika.Kama hali ya uhalifu inashamiri hakuna haja wao kuendelea na nafasi hizo 
IGP Sirro


ANGALIA TAARIFA KAMILI👇👇👇 


 

Post a Comment

0 Comments