MALIASILI YAZINDUA SIMU 14 KURIPOTI UVAMIZI WA WANYAMA

 


 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

WAZIRI wa Maliaasili na Utalii Dkt Damas Ndumbalo amezindua namba maalumu na kugawa simu 14 kwa wakuu wa hifadhi zitakazo tumika kwa ajili ya mawasiliano na wananchi pindi wanapo vamiwa na wanyama wakali

Akizungumza katika hafla fupi leo jijini hapa na wakuu wa hifadhi  Ndumbalo amesema katika kutekeleza ilani ya Chama  cha mapinduzi (CCM)  na kupunguza migogoro kati ya wanyama na binadamu na itakuwa njia rahisi ya kumsaidia mwananchi kuwasiliana na mamlaka husika muda wowote wanapopata matatizo.

Amesema kuwa kutokana na changamoto ambazo zimekuwa zikiripotiwa za kuwepo  wanyama wakali na waharibifu kwa wananchi wanaoishi maeneo yanayo zunguka kwenye hifadhi mbalimbali hapa nchini ,simu hizo zitawekwa kwenye vituo hususani TAWA ,TANAPA,NGORONGORO ,na Wizarani zitasaidia kupata msaada kwa haraka kwani wengi walitoa taarifa hizo wizarani lakini kwa sasa itakiwa vituo maalumu.

"Wizara ya maliasili na Utalii tumezindua hii namba maalumu na simu za kiganjani 14 kwenye hifadhi mbalimbali ,lengo ni kuwasaidia wananchi wanyonge waweze kuwasiliana bure na gharama hizo zitalipwa na wizara na kufanya hivyo itarahisisha utendaji kazi kwa watumishi ambao watafika eneo husika kuwarudisha wanyama hao hifadhini tofaufi na hapo awali"amesema Ndumbaro.

Amewataka watumishi hao kuchapa kazi usiku na mchana kutatua kero za wananchi huku wakitoa hamasa juu ya namba hizo ili kuondokana na madhara yanayojitokeza huku akiwasihi wananchi kutumia namba hizo kwa ajili ya malengo mahususi  ,kutoa taarifa na sio kwa ajili ya kusalimia jambo ambalo sio sahihi.

Naibu waziri wa Mali asili na utii Mary Masanja amesema kuwa wizara kupitia watumishi wake imekuwa ikitoa elimu kwa wananchi namna ya kujikinga na wanyama hao na waharibifu ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha kulima mazao ya pilipili na ufugaji nyuki pembezoni mwa hifadhi ambavyo ni adui kwa wanyama hususani Tembo wanapohisi harufu.

Katibu Mkuu wizara hiyo ya Mali asili na utalii Dkt Allan Kijazi amesema  kuwa changamoto ya mawasiliano ilikuwepo muda mrefu mbali na jitihada mbalimbali kufanyika  kutokana na mawasiliano kuwa mabovu kwani mpaka watumishi wanafika eneo la tukio tayari madhara talikuwa yameisha tokea.

"Tunashukuru Waziri kwa kushirikiana na wananchi inaonyesha ni kiasi gani wizara imejipanga kupunguza hizi kero sisi tuko tayari kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha tunasaidia wananchi na kunusuru maisha yao tuwahahakikishie simu zitakuwa hewani muda wote"amesema  Dkt Kijazi.

Kwa upande wake Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro Dkt Fredy Manongi alisema  kuwa hizo simu zitasaidia kurahisha mawasiliano kwani kila siku upokea simu nyingi kutoka vijiji vilivyopo pembezoni mwa hifadhi ya ngorongoro kutokana na wanyama hao wakali Tembo na nyati ambao wamekuwa tishio.

 

Post a Comment

0 Comments