📌JOHN BANDA
MBUNGE wa jimbo la
Bahi Mkoani Dodoma Kenneth Nollo amesema amejizatiti kupitia mfuko wa jimbo na
michango ya wadau wengine kukamilisha ujenzi wa zahanati 10 kati ya 16
zanazohitajika ifikapo mwaka 2025
Akiongea jimboni humo
na waandishi wa habari Mbunge huyo amesema kuwa kukosekana kwa huduma za afya
kwenye vijiji hivyo 16 kumekuwa kukiwasababishia usumbufu mkubwa wananchi ambao
wamekuwa wakienda umbali mrefu kutafuta huduma hiyo
Nollo amesema ndani ya
miaka mitatu na nusu kuelekea mwaka 2025 atahakikisha anaondoa usumbufu huo kwa
kujenga zahanati katika vijiji 10 ambapo mpaka sasa tayari ameshatoa million 30
kupitia mfuko wa jimbo kwenye vijiji vya Nchinila,Nguji na chikopelo.
Amesema hata hivyo
kupitia zaira ya aliyekuwa rais wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli akitokea
jijini Arusha miezi michache kabla ya kifo chake alitoa Million 50, kwa ajili
ya kumalizia ujenzi wa zahanati ya Mayamaya ambapo serikali pia imetoa kiasi
kama hicho katika vijiji vya Chali na Nchinila.
Hadi sasa kiasi cha million 30, zimeshatolewa toka mfuko wa jimbo kwa ajili ya ujenzi wa zahanati za vijiji vya nchinila, Nguji na Chikopelo huku serikali ikimalizia ujenzi huo kwa million 50 kwa kila kijiji.
Keneth Nollo
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa CCM wilayani Bahi Stewart Masima amempongeza Mbunge huyo kwani
amekuwa akijitoa kwenye kuchangia maendeleo ya wananchi kwa hali na mali
Amesema tangu mbunge
Nollo aingie madarakani kwa kushilikiana na wadau wengine amekuwa akifanya
mengi ya kimaendeleo yakiwemoujenzi wa shule na zahanati pamoja na kukisapoti
chama cha mapinduzi kwenye maswala mbalimbali
“Mbunge kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali amekuwa akifanya mambo mengi ambapo hata sasa
tunasubiri mifuko 500 ya Sumenti kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa zahanati
katika vijiji vingine”, amesema
|
|
0 Comments