MBUNGE JIMBO LA BAHI AWATAKA VIONGOZI KUHAMASISHA KAZI ZA MAENDELEO

 


📌JOHN BANDA

MBUNGE wa jimbo la Bahi mkoani Dodoma Kenneth Nollo (CCM) amewashauri viongozi wa Chama hicho na wale wa Serikali wilayani humo kuendelea kuwahamasisha wananchi ili waendelee kufanya kazi za maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati

Pia amesema katika wilaya hiyo kuna upungufu wa zahanati 16 ambapo ifikapo mwaka 2025 atahakikisha zahanati 10 zinakamilika ili kuwasogezea huduma za kiafya wananchi wanaoishi katika kata za wilaya hiyo

Mbunge huyo aliyasema hayo mara baada ya kukamilika kwa uchaguzi mdogo wa nafasi ya katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho wilayani bahi uliofanyika baada ya aliyekuwa akiishikilia kuchaguliwa udiwani kata ya chali na baadae kuchaguliwa kuwa Makamu mwenyekiti wa Halmashauri, ambapo Nasson Kachinda aliibuka mshindi

Nollo alisema ili kuhalakisha maendeleo ya wilaya hiyo ni vizuri kuwe na ushirikiano kati ya viongozi wa CCM na wananchi ili kuweza kuibua kero zilizopo ili iwe rahisi kuzifikisha serikalini ambako zitafanyiwa kazi kwa ajili ya maendeleo ya wilaya hiyo

Viongozi wa chama mkishirikiana vizuri na wananchi mtaibua kero nyingi na zenye tija ambazo zikifikishwa na kufanyiwa kazi serikalini wilaya yetu itapaa kimaendeleo

Aidha aliwataka viongozi kuendelea kuwahamasisha wananchi ili waendelee kujitolea kwenye kazi za maendeleo na hasa nguvu kazi kwenye ujenzi wa zahanati ambazo yeye kama mbunge wao pamoja na wadau wengine wamekuwa wakitoa mifuko ya sumenti kwa ajili ya ujenzi    


                Katibu wa Itikadi na Uenezi Wilaya ya Bahi Nasson Kachinda akiozungumza 
                               jambo mara baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.

Alisema kwa upande wa serikali mpaka sasa imeshatoa  million 150 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa zahanati za Chikopelo, Mayamaya na Mkakatika ambako wananchi walitolea nguvu kwa kwa bidi kubwa

“viongozi endeleeni kuwahamasisha wananchi waendelee kujitolea nguvu zao kwa kufanya kazi za maendeleo, hasa kukusanya mawe na mchanga pamoja na kuchimba misingi ili zahanati zijengwe

Naishukuru serikali ambayo kutokana na maendeleo mazuri ya ujenzi wa zahanati za chikopelo, Mkakatika na mayamaya wameshatoa million 150 inayogawanywa kwenda kumalizia zahanati hizo tatu”, alisema Nollo

Aliongeza kuwa mpaka sasa kupitia mfuko wa jimbo tayari ameshato million 30 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati za Nguji, njinia, na chikopelo ambapo ifikapo mwaka 2025 atakuwa amekamilisha 10 kati ya 16 zinazohitaji

Mwenyekiti wa CCM wilayani bahi Stewart Masima akiongea katika uchaguzi huo alisema tangu amekuwa mwenyekiti hajawahi kupokea msaada toka kwa mbunge ambapo hata gari la chama walikuwa wanaliogopa kulitumia kutokana na matairi yake kuwa vipara lakini mbunge amesha nunua yote manne na gari limeanza kutumika  

 


Post a Comment

0 Comments