RAIS MWINYI AKUTANA NA SAKHO WA CRYSTAL PALACE,AMPONGEZA

 


📌MWANDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar Mhe. Dk. Hussein Mwinyi akutana na Mchezaji wa Crystal Palace, Ikulu Jijini Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameipongeza azma ya Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu wa Klabu ya Crystal Palace inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL) Mamadou Sakho ya kuanzisha kituo cha kuendeleza vipaji vya michezo kwa vijana hapa Zanzibar.

Rais Dk. Mwinyi alitoa pongezi hizo leo Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu wa Kilabu ya Crystal Palace inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL) ambaye pia ni Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Mamadou Sakho.

Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Mwinyi alieleza kwamba azma hiyo ni mwanzo mzuri katika kuinua na kuendeleza vipaji vya michezo vya vijana wa Zanzibar.

Rais Dk. Mwinyi alimpongeza Mamadou kwa kuitembelea Zanzibar kwa mara ya pili kutokana na mazingira pamoja na watu wa Zanzibar na utamaduni wao.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alimueleza mchezaji huyo wa timu ya Crystal Palace kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kushirikiana nae katika kuanzisha kituo hicho cha kuendeleza vipaji vya michezo kwa vijana hapa Zanzibar.

Rais Dk. Mwinyi alimueleza mchezaji huyo kuwa ujio wake una umuhimu mkubwa katika kuutangaza utalii wa Zanzibar pamoja na vivuto vilivyopo.


Nae Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu wa timu ya Crystal Palace inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL) ambaye pia ni Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Mamadou Sakho alimueleza Rais Dk. Mwinyi azma yake ya kuanzisha kituo cha kuendeleza vipaji vya michezo kwa vijana hapa Zanzibar.

Mamadou ambaye amefuatana na Mkewe Majda Sakho, alisema kuwa ameamua kuchukua hatua hiyo ya kuanzisha kituo cha kuendeleza vipaji vya michezo kwa vijana hapa Zanzibar kwa kutambua kwamba ana deni na wajibu mkubwa wa kuleta maendeleo Afrika akijuwa kwamba yeye ni Mwafrika licha ya kwua amezaliwa Ufaransa na anabeba uraia wa Taifa hilo.

Aliongeza kuwa ameichagua Zanzibar kuwa ni eneo maalum kwa kuanzisha kituo hicho kitakachoendeleza soka hapa nchini.

Post a Comment

0 Comments