📌MWANDISHI WETU
RAIS wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hussein Ally Mwinyi ameipongeza tume ya Haki za Binadamu na utawala bora kwa kuanzisha mfumo mpya wa kushughulikia malalamiko ya wananchi kwa njia ya mtandao.
Aidha ameitaka tume hiyo kuongeza nguvu na kulipa kipaumbele eneo hilo kwani litaokoa muda wa wananchi katika utatuzi wa kero zao.
Ameyasema hayo jana
mjini Zanzibar wakati wa mazungumzo kati ya Tume ya Haki za binadamu ya kwenda
kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais na kuitambulisha Tume na majukumu
yake,mafanikio, changamoto, na kuomba muendelezo wa ushirikiano
kutoka kwenye wizara,idara,na taasisi za serikali.
Naipongeza sana Tume hii na nitashirikiana nayo kwa asilimia mia moja ili kuiwezesha na kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa katiba.
Rais Mwinyi
Naye mwenyekiti wa Tume ya haki za binadamu Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amempongeza Rais Mwinyi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar kwa kuendeleza Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ambayo imepata mapokeo chanya kutoka kwa wananchi.
"Nisema tu kwamba hatua za kufikia uchumi wa blue, ili kuhakikisha kuwa wananchi wa Zanzibar wanafaidika na matumizi stahiki ya maliasili ya bahari kwa shughuli za biashara ya uvuvi, usafirishaji, na kilimo cha zao la mwani , kwa kuimarisha Haki za Binadamu na Utawala Bora na kuongeza dhana ya uwazi,uwajibikaji,ushirikishwaji usawa na ushughulikiwaji wa malalamiko naomba nikupongeze sana Mhe Rais"amesema Jaji Mwaimu.
Sambamba na hayo amesema wanafurahishwa kuona wananchi, kwa kuchukua hatua za kuanzisha mfumo wa kuwasilisha malalamiko moja kwa moja kwa Rais unaojulikana kama SEMA NA RAIS MWINYI (SNRMWINYI).
"Kitendo cha kuanzisha mahakama maalum ya kushughulikia kesi za udhalilishaji, na utaratibu wa kusikiliza changamoto za makundi mbalimbali kama vile wanawake, wazee, na wenye ulemavu, na kwa kuimarisha mapambano dhidi ya Rushwa kwa kuboresha Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar, kwa kusimamia mapato na matumizi sisi kama tume ya haki za binadamu tumefurahishwa sana" amesema Mwaimu
Sanjari na hayo Tume imetambulisha Majukumu yake kwa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na kuelezea ofisi zilipo bapa nchini.
"Tume ina ofisi Dodoma (Makao Makuu, Unguja, Pemba, Dar es Salaam, Mwanza, na Lindi. Na kwamba Tume inatarajia kufungua Ofisi Mbeya na Tabora, na nikujulishe Mheshimiwa Rais kuwa Majukumu ya Tume ni kuhamasisha ulinzi na uhifadhi wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa kutoa elimu kwa jamii juu ya masuala ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora,
"Kwa kufanya tafiti na uchunguzi wa malalamiko pale kunapodhaniwa kuna uvunjifu wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora kupendekeza sheria zenye changamoto katika kuzingatia haki za binadamu na utawala bora kuishauri Serikali juu ya masuala ya haki za binadamu na utawala bora,kushirikiana na asasi binafsi na taasisi za serikali katika kutatua changamoto za wananchi" amesema Mwaimu
Hata hivyo Jaji Mwaimu
amesema kazi ya tume nyingine ni kuandaa ripoti juu ya hali ya haki za
binadamu na utawala bora nchini pamoja na changamoto zake, na kuonesha hatua za
maboresho ya utatuzi wa changamoto husika zilizochukuliwa na
serikali.
0 Comments