TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUTUMIA MIFUMO ILIYOTENGENEZWA NA KUSIMAMIWA NA MAMLAKA YA SERIKALIMTANDAO (eGA)




 ðŸ“ŒMWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Mohamed Mchengerwa amewaonya wakuu wa Taasisi za umma nchini wenye lengo la kujitoa katika matumizi ya mifumo iliyotengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) na kusema kuwa kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa Sheria

Mhe.Mchengerwa ameyasema hayo jijini Dar es Salaama wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea ofisi hiyo na kuzungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo ya Serikali Mtandao

''Ninafahamu kuna baadhi ya Taasisi za Serikali kushirikiana na wadau wao wanaotaka kujitoa katika matumizi ya mifumo inayotengenezwa na eGA,kujitoa katika mifumo ambayo tayari tumeirasimisha kwa misingi ya sheria ya Serikali Mtandao namba 10 ya mwaka 2019 na kanuni zake za mwaka 2020 ni kinyume cha Sheria''Alisema Waziri wa Mchengerwa

Nitoe rai na onyo kwa wakuu wote wa Taasisi za Serikali kuwa hakuna Taasisi wala Ofisi yoyote ya Serikali ambayo inaruhusiwa kujitoa kwenye mifumoinayosimamiwa na eGA

Waziri Mchengerwa

Aidha pia ameiagiza eGA kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhakikisha wanadhibiti  uvujaji wa siri lakini pia utolewaji wa taarifa ambazo hazistahili kwenda moja kwa moja kwa watumiaji wa kawaida

Vile vile ameipongeza eGA kwa  jitihada kubwa wanazofanya za kuendelea kubuni mifumo ambayo ina rahisisha utendaji kazi Serikalini ambapo pia amewasihi kuendelea kutekeleza jukumu hilo kwa kuzingatia kasi ya Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) Mhandisi Benedict Ndomba yeye ametaja baadhi ya athari zinazoweza kujitokeza endapo Taasisi za umma hazitopeleka taarifa za mifumo inayoanzisha kuwa ni pamoja na kutokufata viwango na miongozo jambo linalopelekea mifumo kutowasiliana

 

Post a Comment

0 Comments