TANZANIA VITANI NA MAREKANI,BRAZIL SOKO LA SOYA;BASHE ATOA MBINU ZA USHINDI

 


📌PENDO MANGALA

 

WIZARA ya Kilimo imekutana na Wadau wa zao la Soya Jijini Dodoma lengo likiwa ni kujadili namna ya kuboresha uzalishaji wa zao hilo na kutatua changamoto ya masoko ya zao hilo.

 Akizungumza katika Mkitano huo,Naibu Waziri wa Kilimo,Hussein Bashe amesema kuwa hivi sasa Tanzania imepata haki ya kuuza zao la Soya nchini China na hivyo kuingia katika ushindania na nchi za Bara la Amerika zikiwemo Marekani na Brazil.

Amefaafanua kuwa hivi sasa mnunuaji mkubwa wa zao la soya ni nchi ya China huku akiwataka Watanzania kuhakikisha wanachangamkia fursa ya soko la zao hilo kwa kuhakikisha wanauza Soya zenye kiwango cha ubora kutokana na ushindani wa soko uliopo hivi sasa.

“Hivi sasa mtumiaji mkubwa wa Soya ni nchi ya China sisi kama Watanzania tuna fursa kubwa yakutumia Soko la china katika kuuza Soya bora ili kuendana na ushindani wa soko kwani kilo moja ya soya nchini China ni Shilingi 3500 ya Kitanzania lazima tuendane na soko,”amesema

 

Mahitaji ya Soya Nchini China ni Tani Mil115 kila mwaka.Wao huzalisha tani 17 tu kwa mwaka. Hata hivyo uzalishaji wetu ni mdogo kama  (tani 14 mwaka 2020/2021).Wizara tutahakisha tunawezesha uzalishaji wa zao la Soya ili kuendana na mahitaji ya soko hilo

Bashe.

 Waziri Bashe  amesema kuwa kama Wizara ya Kilimo watashirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali wa kilimo katika kuhakikisha biashara wanazouza zinakuwa na ubora ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananufaika na biashara zao.

Lengo la Wizara ni kuhakikisha wafanyabiashara wanakuwa wawekezaji wakubwa ambao wanauza bidhaa zenye ubora nje ya nchi ili kuendana na mahitaji ya ushindani wa masoko.

Hata hivyo amevitaka vituo vya utafiti wa Mbegu nchini kuhakikisha vinafanya utafiti wa mbegu ili kuweza kuzalisha Mbegu zenye ubora.

Katika hatua nyingine amewataka wafanyabiashara ambao wanaenda nje ya nchi kwaajili ya kufanya biashara kuhakikisha wanafika katika balozi zao kujitambulisha kwa lengo la kusaidiwa na balozi zao pale linapotokea tatizo lolote.

Mkifika katika ubalozi wenu katika nchi mnazoenda kwaajili ya kibiashara,huduma zote ni bure na hamtadaiwa fedha yeyote na wala pale sio kituo cha polisi wala  sio TRA.Kuwa karibu na balozi hzetu nje ya nchi inawasaidia kuwalinda ninyi katika shughuli zenu huko nje ya nchi.

Bashe


Post a Comment

0 Comments