TMDA KANDA YA KATI YATAKIWA KUENDELEA KUTOA ELIMU JUU YA MADHARA YA MATUMIZI MABAYA YA DAWA.

 


📌SALEH RAMADHANI 

MAMLAKA ya dawa na vifaa tiba  (TMDA) mkoani Dodoma imekumbushwa kuendelea kutoa elimu  kwa jamii juu ya matumizi mabaya ya dawa na vifaa tiba.

Akizungumza  katika mafunzo maalumu juu ya matumizi ya dawa,  Kaimu katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma Aziza Rajabu Mumba  amesema lengo kubwa la kutoa mafunzo kama hayo  ni kuhakikisha   kupuguza madhara makubwa juu ya athari za dawa kwa watumiaji.

Mafunzo haya ni muhimu sana kwa watoa huduma za afya hivyo,niipongeze TMDA kanda ya kati kwa kuwezesha mafunzo haya na nina uhakika watakaonufaika na mafuzo haya italeta tija kubwa katika utoaji wa huduma kwa mwananchi 

Kaimu katibu tawala huyo wa mkoa  ametoa wito kwa mamlaka ya dawa na vifaa tiba(TMDA)kuendelea kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya dawa na vifaa tiba.

“Wito wangu ni kwa mamlaka kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kuelewa vifaa tiba na dawa tunazotumia mbali  matokeo chanya lakini vinaweza kuwa na matokeo hasi ,taarifa ziende kwa haraka  ili kudhibiti matumizi ya dawa ambazo zina madhara kwa mwanadamu na suala hili ni pan asana hivyo elimu inahitajika zaidi”amesema.

Katika hatua nyingine  amesema  kwa sasa hali sio mbaya  hasa kwenye eneo la madhara ambapo , mambo yamekuwa mazuri, kutokana na elimu kuendelea   kutolewa kila wakati kwa jamii kuhusiana na utumiaji wa dawa na vifaa tiba katika afya ya mwanadamu.

Kwa upande wake kaimu meneja wa mamlaka ya dawa na vifaa tiba[TMDA]   kanda  ya kati  Sonia Henry amesema mafunzo hayo dhima yake kubwa ni kuwakumbusha watoa huduma katika majukumu yao ili kuwa makini katika kutoa huduma inayostahili na kulinda afya ya jamii .

“Mafunzo haya yanalenga kutoa elimu kwa watumishi wa sekta ya afya kutoka katika halmashauri  mkoa wa Dodoma , kuwakumbusha msingi mkubwa wa utoaji wa taarifa kwani utoaji wa taarifa unasaidia kuokoa maisha ya mwanadamu na mara tupatapo taarifa papo hapo tunachukua hatua katika kumlinda mwananchi ili asidhurike na dawa ama vifaa tiba  ambavyo ni hatarishi”amesema.

Aidha,amebainisha kuwa zaidi ya watumishi 30  kutoka kila halmashauri mkoani Dodoma wananufaika na mafunzo hayo katika kuwajengea  uwezo .

 

Post a Comment

0 Comments