UVCCM YAENDELEA 'KULIA' NA GHARAMA ZA BANDO


 

📌RHODA SIMBA

KATIKA kuwepo kwa malalamiko ya wananchi kuhusu kupanda kwa gharama za vifurushi  Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umeishauri Serikali kuona haja ya kuangalia upya suala la huduma za vifurushi.

Hayo yamesemwa leo jijini hapa na katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Raymond Mwangwala  wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza kuu la umoja wa vijana CCM.

Aidha ameishauri Serikali kuona haja ya kuangalia upya suala la huduma za vifurushi  kwa kulichukulia kwa umakini ili kuokoa ajira kwa vijana waliojiajiri katika uchumi wa kidigitali.

Sisi kama vijana wa CCM  tunaishauri  serikali ,vijana wetu wanaelekea kukosa ajira kutokana na gharama kubwa za bando,tunaiomba Serikali yetu tukufu kuona namna ya kuboresha changamoto ya huduma za vifurushi kupitia mitandao ya simu

 Kwani uwepo wa gharama za juu katika manunuzi hukwamisha vijana kukua kiuchumi kutokana  na wengi kufanya shughuli zao kupitia mitandao ya kijamii,"amesema

 

 Pia baraza kuu limemvua uongozi Hussen Salehe aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM wa wilaya ya Moshi vijijini kwa kutokuwa na maadili pamoja na nidhamu baada ya kupokea mapendekezo yaliyowasilishwa katika kikao cha halmashauri kuu ya CCM ya mkoa wa Kilimanjaro.

"Baraza kuu lilijiridhisha,Kamati ilijiridhisha na kuona kwamba kwa tuhuma zile na mapendekezo yaliyotolewa katika kikao halmashauri kuu ya mkoa hivo limemvua uongozi,

“Hivyo naagiza mkoa wa Kilimanjaro kutangaza nafasi  ya mwenyeki wa uvccm, katika wilaya ya moshi vijijini”amesema.

 Sambamba na hayo UVCCM pia imeazimia kumuenzi hayati Dkt. John Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano kwa kuyaendeleza yale yote mazuri aliyoyafanya katika kipindi cha uongozi wake.

Lakini pia wamempongeza Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuteuliwa kwa ushindi mnono huku akiwawataka vijana kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Samia pamoja na serikali yake.

Tutamlinda ,tutamtetea Rais wa chama chetu iwe mvua au jua,pia kwa kuongeza juhudi katika kufanya kazi na uzalendo katika nchi yetu

Pia wamempongeza Daniel Chongolo pamoja na wajumbe wote walio chaguliwa kuunda sekretarieti mpya ya chama chetu,tunaimani kubwa nao,tupo tayari kushirikiana nao kwa maslahi ya chama chetu kwa kazi nzuri pia tunakiopongeza chama chetu kwa kazi nzuri ya kusimamia cham,a chetu.

“Sisi kupitia wawakilishi wetu wa ngazi mbalimabli za maamuzi tunaendelea kusimamia serikali na hususani kupitia vijana wakiwa bungeni,kusimamia serikali kuhakikisha inatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kwa maslahi ya vijana na taifa kwa ujumla.

 


Post a Comment

0 Comments