WAZIRI JAFO ATEUA MABALOZI WA MAZINGIRA,WAANDISHI CPC KUUNGANA NA DIAMOND ,HARMONIZE

📌RHODA SIMBA

 

WAZIRI wa Nchi ,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo  ameteua  Wajumbe14 washauri pamoja na mabalozi 40 wa kampeni ya Mazingira yenye  lengo la kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi shindani Duniani katika  kutunza Mazingira.

Aidha katika orodha ya mabalozi hao imejumuisha waandishi wa habari Sakina Abdulmasoud,Aboubakari Famau,pamoja na Oliver Nyeriga  ambao ni wanachama wa klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Dodoma ( CPC) .



Sakina Abdul Masoud mwandishi kutoka Uhuru Media Groupambaye pia ni mwanchama
 wa Central Press Club ni miongoni mwa mabalozi 40 walioteuliwa na Waziri Jafo.


 Akizungumza na Waandishi wa Habari leo  Waziri huyo amesema kampeni hiyo imekuja baada ya maeneo kama vile maziwa na bahari kiwango cha maji kimepanda kutokana na uchafuzi wa mazingira katika maeneo hayo.

Kampeni hii ya Mazingira kwa Mwaka huu itahusisha kila Idara,zikiwemo Taasisi,Mikoa pamoja na Wilaya,kata vijiji na Mitaaa,Viwanda migodi na maeneo mbalimbali wakiwemo wadau wa Usafi na itaungana na utoaji wa tuzo mbalimbali kwa Washindi wa uandishi wa Habari za Mazingira 

Waziri Jafo.

 Na kuongeza kusema "Washindi 152 wa tuzo hiyo watapata nafasi yakwenda kutaliii katika Mbuga ya wanyama ya Mwalimu Nyerere na niwambie waandishi wa habari safari hii kuna zawadi kabambe zitatolewa kutokana na siku hii ya mazingira",amesema 

Amesema kampeni hiyo ya Mazingira yenye kaulimbiu isemayo Mazingira yangu,Tanzania Yangu,Nakupenda Daima  itazinduliwa rasmin June 5 mwaka huu siku ya Kilele Cha maadhhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambapo  mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais DK.Philip Mpango Mkoani Dodoma huku akisema  kampeni hiyo itakuwa endelevu.

 Aidha Wajumbe14  ambao aliwateua kushauri mwendo wa kampeni,uteuzi wa majaji ili kuhakikisha kampeni inapata mafanikio makubwa kuwa ni Seif Ally Seif Mkurugenzi wa Superdoll ambaye ni Mwenyekiti, Andrew Komba ni Katibu anatoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Dosantos Silayo Kamishina wa TFS  

Nana tarajia kukutana na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayohusika na mazingira mnamo mei 27 Jijini Dodoma kwa lengo la kuiwezesha kampeni hiyo.

 Hata hivyo Mabalozi 40 aliowateua wakiwemo wasanii pamoja na Waandishi wa Habari akiwemo Msanii Diamond platnums na Harmonize.

 

Post a Comment

0 Comments