WAZIRI WA KILIMO AAGIZA KUSIMAMIAHWA KAZI KWA MRAJIS MAAIDIZI WA LINDI

 


📌PENDO MANGALA

 

WAZIRI wa Kilimo Prof.Adolf Mkenda amemuagiza Mrajis  na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini Dkt Benson Ndiege  kumsimamisha kazi Mrajis Msaidizi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Lindi  Edmund Masawe kutokana na kukilazimisha Chama cha Ushirika wa mazao (AMCOS) cha Umoja kilichopo Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi kukodi ghala binafsi kwa ajili ya kuhifadhia Korosho wakati chama hicho kina ghala lake la kuhifadhia korosho.

Waziri Mkenda ametoa agizo hilo   jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Jijini Dodoma huku akieleza kuwa Wizara hiyo itaendelea kuunganisha nguvu ya wakulima kwa kutumia ushirika.

Akieleza zaidi Mkenda alimtaka Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini Dkt Benson Ndiege kujitathmini kutokana na kushindwa kutekeleza ahadi ya kutoa ushauri wake alioelekezwa wakati wa kikao cha majadiliano kilichofanyika tarehe 8 Mei 2021.

"Unajua watu hawako seriazi ,katika kikao kazi tulichokaa Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini aliagizwa kutoa taarifa ya ushauri wake kuhusu Mradi wa pamoja wa vyama 32 vya msingi vya Ushirika (G32) vya Mkoani kilimanjaro lakini hakufanya hivyo;

Katibu Mkuu Mimi nadhani Mrajis wa Vyama vya Ushirika anafanya mzaha, Anadhani siwezi kumng’oa na pengine mahali pa kuanza kupafumua katika Wizara ya Kilimo ni Tume ya Maendeleo ya Ushirika

Prof.Mkenda

 

Licha ya hayo Prof Mkenda alisema kuwa amemuweka Mrajis na mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya ushirika katika uangalizi maalumu huku akimuagiza kufika Jumatatu tarehe 17 Mei 2021 kuwasilisha mapendekezo hayo haraka iwezekanavyo.

"Wach out,nitachukua hatua kwa ajili ya kuboreshà ushirika,nimekabidhiwa kuingoza Wizara ya Kilimo ili kuimarisha sekta ya Ushirika nchini ikiwa ni pamoja na kuongeza uzalishaji na tija kwa wakulima,lakina kuna wengine bado wanafanya mzaha,"alisema.

Aidha,Waziri huyo mwenye dhamana ya Kilimo alizungumzia kuhusu kadhia iliyoikumba Tanzania Kuhusu Nzige wa Jangwani na kusema  kuwa kati ya tarehe 14 Januari, 2021 na 24 Februari, 2020 Tanzania ilipata uvamizi wa Nzige wa Jangwa waliotokea nchi jirani ya Kenya na kuingia katika Wilaya nane (8) za Mwanga, Siha na Moshi (Kilimanjaro), Simanjiro (Manyara) huku akifafanua kuwa Serikali imeshachukua hatua kudhibiti uhalibifu.

Aliyataja Maeneo mengine kuwa ni Longido, Monduli na Ngorongoro (Arusha); na Lushoto (Tanga) na kwamba Kati ya Wilaya hizo, nzige walikuwa wakihama kutoka kwenye maeneo waliokuingia na kulala maeneo mbalimbali ya Wilaya nne (4) Siha (Kilimanjaro), Simanjiro (Manyara); Longido na Monduli (Arusha) wakitanda kwenye eneo la jumla ya hekta 6,441.

Katika hatua nyingine Waziri huyo ameunda Jopo la wataaalamu ambalo litasimamiwa na Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kwa lengo la kutatua changamoto za Masoko ya Kilimo.MWISHO

 

Post a Comment

0 Comments