CHAVITA YATAKA MTAALA MAALUM WA VIZIWI SHULENI


 ðŸ“ŒDOTO KWILASA

CHAMA cha Viziwi Tanzania(CHAVITA) kimeilalamikia Idara ya Elimu nchini kwa kushindwa kuwa na mtaala maalumu wa kufundishia wanafunzi viziwi mashuleni na kusababisha kushindwa kuendelea na Elimu ya juuu.

Hayo yamesemwa leo hii Jijini hapa na Mkurugenzi Mtendaji CHAVITA Dickson Mveyange wakati akizungumza kwenye mafunzo na kampeni kuhusu ukiziwi na lugha ya alama yaliyohusisha wadau wa Elimu,wazazi wa watoto wenye ukiziwi na wadau wa maendeleo.

Amesema,mitaala inayotumika mashuleni ni ya jumla na haiwazingatii viziwi Pamoja na kuwa kina tofauti ya wanaosikia na viziwi  hali ambayo ni kikwazo kwa watoto hao ambao wanatakiwa kupewa Elimu maalum badala ya Elimu ya jumla.

Licha ya hayo Mkurugenzi huyo amesema,licha ya Idara ya maendeleo ya Jamii kuridhia kuwepo kwa lugha ya alama lakini inaonekana Jambo hilo bado halijatekelezwa ipasavyo na kusababisha wanafunzi wengi viziwi kushindwa kuendelea na masomo Kutokana na ugumu wa lugha ya Mawasiliano.

Bado Kuna mapungufu mengi,tunahitaji maboresho zaidi ili kuweka usawa kwa jamii na viziwi nao waweze kusoma bila kubaguliwa,bado ukosefu wa misamiati ya masomo ya sayansi, uraia na historia  bado ni  changamoto,vitu vyote hivi vinapaswa kuangaliwa upya

Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa Mtaala uliopo unawanyima wanafunzi  fursa ya kufikia malengo yao katika masomo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama hicho Nidrosy Mlawa aliitaka jamii kuwashirikisha viziwi kwa mambo yote ili maendeleo yasimwache mtu.

Amesema,ili kuifikia Tanzania ya ndoto za walio wengi lazima kuwepo marekebisho Katika mitaala ya Elimu ili watu wenye mahitaji maalumu wasibaki nyuma.

Kuna hili suala la  ufinyu wa muda katika vipindi, sehemu kubwa ya wanafunzi wenye uziwi hawawezi kumaliza maswali katika majaribio ya saa moja na nusu kwa sababu ni ngumu sana kwao kusoma sentensi ndefu na hata kwenye hesabu swali moja la kufanya dakika mbili wao hutumia dakika tano ili waweze kupata jibu sahihi.

Amesema,Mtaala wa elimu ni mwongozo wa masomo unaotoa dira ya mafunzo yanayotakiwa katika utoaji wa mafunzo kwa wanafunzi katika ngazi fulani ya elimu

Kutokana na hayo Baadhi ya walimu wanaowafundisha wanafunzi wenye uziwi walitumia nafasi hiyo pia kueleza changamoto wanazokutana nazo wanafunzi hao wawapo shuleni huku wakiiomba Serikali kulivalia njuga suala hilo ili kuweka usawa.


Mwalimu Marry Masangula kutoka  shule ya msingi Kigwe-Viziwi Dodoma,ameeleza kuwa  wa sasa wanafunzi wenye uziwi hutumia mda mwingi hadi kumaliza elimu yao ya msingi kutokana na kutokuwepo kwa miundombinu  sahihi kuwawezesha kuelewa masomo.

Amesema, ili kumaliza elimu yao ya shule ya msingi kunakuwa na vikwazo vingi Sana ukikinganisha  na wanafunzi wasio walemavu ambao hutumia miaka saba tu kumaliza elimu hiyo.

"Ili waelewe vyema wanafunzi wenye uziwi kama sisi walimu tunapaswa kutumia zaidi lugha ya alama pamoja na vitendo kuwaelimisha lakini Jambo hili bado ni gumu kwa kuwa walimu pia hawatoshelezi,"anasema

Amesema,Kwa kawaida ratiba iliyopo kwenye mtaala wa sasa inampa mwalimu dakika 40 tu za kufundisha ikiwa ni muda sawa kwa wanafunzi wote wa shule ya msingi wenye mahitaji maalum na wasio walemavu,Dakika ambazo  zaelezwa kutotosha kuwafundisha watoto hao wenye mahitaji maalum.

Post a Comment

0 Comments