KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA MAENDELEO JESHI LA MAGEREZA




 ðŸ“ŒMWANDISHI WETU

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na usalama imeridhishwa na maendeleo yanayofanywa na Jeshi la Magereza ikiwa ni utekelezwaji wa maono ya aliyekuwa rais wa awamu ya sita hayati Dkt.John Magufuli,aliyelitaka jeshi hilo kujitegemea.

Akizungumza baada ya ziara fupi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na jeshi hilo katika makao makuu yake katika eneo la Msalato jijini Dodoma,Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mussa Azan Zungu alisema hatua iliyofikiwa na jeshi hilo ni ya kupongezwa.

Katika ziara hiyo Kamati ilitembelea kiwanda cha samani ambacho hadi ukamilikaji wake kimegharimu takribani shilinig bilioni 2, nyumba za askari 150 wa jeshi hilo pamoja na majengo ya Makao Makuu.

Ni kazi nzuri imefanywa na Meja Jenerali wa Magereza Suleimani Mzee,tulipokuja hapa (Msalato) mwaka jana tulipouona msingi wa jingo la kiwanda cha samani hatuona matumaini ya kukakimilika kwake,lakini tunarudi baada ya mwaka kimekamilika.

Zungu.


Kamati hiyo ilibainishwa kwamba licha ya serikali kupunguza kupeleka fedha kwa ajili ya chakula katika jeshi la Magereza lakini jeshi hilo halijateteleka hivyo hiyo ni ishara tosha kwamba katika miaka michache ijayo linaweza kujiendesha lenyewe bila kutegemea ruzuku ya chakula kutoka serikalini.

Zungu pia amesema katika maagizo 6 waliyotoa katika ziara ya mwaka jana,Uongozi wa jeshi hilo umeyatamiza kwa ufanisi  ikiwemo ujenzi hospitali na  karakana ya utengenezaji wa magari ili kupunguza mzigo kwa serikali.

“Tuliwaagiza pia waanzishe karakana na leo tumeiona imekamilika.Hii itaisaidia kupunguza mzigo wa matengenezo ya magari ambayo huwa yanapelekwa kwenye karakana binafsi kwa ajili ya matengenezo.” Alibainisha Zungu.



Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Kamishna Jenerali wa Magereza Meja Jenerali Suleimani Mzee alisema hatua ya jeshi hilo kujitegemea imepunguza madeni kutoka kwa wazabuni waliokuwa wanatumika kulisha wafungwa na askari wa jeshi hilo.

Kamishna Jenerali Mzee alibainisha kuwa kabla ya kujitegemea serikali ilikuwa inatoa kiasi cha takribani milioni 800 hadi 900 kwa ajili ya chakula tangu waanze kujitegemea mwezi Machi mwaka 2020. Pia amewahakikisha Kamati hiyo kwamba samani zitakozalishwa katika kiwanda hicho zitakuwa zenye ubora na bei itakuwa nafuu ili kila Mtanzania aweze kumudu hali itakayoiongezea kipato cha uhakika jeshi hilo.

Post a Comment

0 Comments