KANISA LAWAONYA VIJANA WANAOWATEGEMEA WAZEE

 


 ðŸ“ŒDOTTO KWILASA         

ASKOFU mkuu na Mwenyekiti wa kanisa la Waadventista Wasabato jimbo la kusini Mwa Tanzania Mch. Mark Walwa  Malekana  ametoa wito kwa vijana kuwa na mpango mkakati  wa kufanya kazi ili kujikwamua kiuchumi na kuachana na dhana ya utegemezi kutoka kwa wazazi.

Mchungaji Malekana amebainisha hayo  jana jijini hapa katika mwendelezo wa mkutano wa shangwe katika njia Yake  ambapo alisema kumekuwepo na kasumba kwa baadhi ya vijana kuwa  na uvivu na kutegemea kwa wazazi ambao ni wazee hivyo ni wakati sasa umefika kwa vijana kufanya kazi kwa bidii.

Aidha,Mchungaji Malekana ametoa hamasa kwa kwa vijana na watanzania kwa ujumla kuacha anasa  na kujikita zaidi kufanya  mambo yampendezayo Mungu.

“Vijana unakuta wapo kwenye vilabu vya pombe wanafanya vitu wa anasa na wanafanya dhambi za kila aina  kwenye baa wananunuliana bia hawajitabui hivyo natoa wito wajinyenyekeze kwa Mungu’’amesema.

Sanjari na hayo Mchungaji Malekana ametoa onyo  kwa baadhi ya washiriki wanafiki wanaotenda matendo maovu kwa kujificha ikiwa ni pamoja na kuvaa nguo zisizo za maadili pamoja na kuvunja shule Sabato ingawa wakiujua ukweli na kusisitiza kutii amri za Mungu.

’’Nawaambia wana wa Afrika fanyeni kazi kwa siku sita  na kuendelea kutii amri za Mungu  na kuvaa mavazi yaliyo na maadili nay a kumpendeza Mungu’’amesema.

Kuhusu suala la uimbaji kanisani,Mchungaji Malekana alitoa wito kwa kwaya zilizo ndani ya kanisa la Waadventista Wasabato kkuimba kwa  kufuata kanuni za uimbaji ndani ya kanisa   huku akitumia fursa hiyo kuipongeza kwaya ya Jangwani kutoka Mkoani Shinyanga kwa kuelendelea kuimba kwa utulivu bila papara.

Katika hatua nyingine Mchungaji Malekana aliwaasa vijana waliopotea kwa kujikita katika dawa za kulevya,uasherati kuona haja ya kurejea kwenye usafi wa moyo.

 

Post a Comment

0 Comments