KIWANDA CHA MBOLEA KUZALISHA AJIRA 3000 DODOMA

 


📌HAMIDA RAMADHANI

KIWANDA kikubwa cha Mbolea kutoka kampuni ya Intracom ya nchini Burundi kinatarajiwa kujengwa Dodoma eneo la Nala ambapo jumla ya watu 3000 watapata ajira za kudumu.

Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Meneja wa Kituo cha uwekezaji (TIC) kanda ya kati  Aboubakari  Ndwata katika ziara ya kukagua shughuli zinazoendelea  kiwandani hapo.

Amesema kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kutoa tani 500'000 za mbolea kwa mwaka.

"Kama tunavyojua tunaagiza mbolea nje karibu tani laki 700,000 hivyo kiwanda hiki katika eneo la Nala kitakuja kuokoa pesa zetu tunazozipeleka nje"amesema Ndwata

Amesema uwekezaji huo utagharimu dola za kimarekani Bilioni 180 ambapo kwa Tanzania ikiwa ni takribani Bilioni 4000 kwa shilingi za Kitanzania.

"Nachukua nafasi hii kumshukuru Rais wa awamu ya sita  Samia Suluhu Hassan baada ya kusema Serikali na Taasisi zake kuboresha fursa za uwekezaji,"

Na kuongeza kuwa " Nawashukuru watoa huduma wa serikali ambao wamewezesha   kama tulivyoona nguzo zimetandazwa kilometa Tano kutoka chanzo cha umeme lakini Shirika la umeme Tanzania limewezesha kuhakikisha umeme umefika"amesema Ndwata

Sambamba na hayo ametoa wito kwa wawekezaji wengine ambao wana maeneo Nala kwenda kuanzisha viwanda kwani umeme na maji yanapatikana muda wote.

"Eneo hili kulikuwa na shida ya umeme na maji ilikuwa ukimleta muwekezaji  huku alikuwa anasema eneo ni porini hivyo shida ya umeme wala maji haipo wawaekezaji wote wenye maeneo waje kufungua viwanda" amesema Ndwata

Naye Mhandisi wa Mradi huo Tumaini  Chonya kutoka Shirika la umeme Tanesco Dodoma amesema mradi huo upo katika hatua ya Mwisho ya kukamilisha ambapo transformer   Yenye ukubwa  wa KVA 500 na nyingine KVA 50 imepita kwenye maeneo ya wananchi Ili waweze kupata umeme.

"Muda sio mrefu laini zote zitakuwa na umeme hapa naweza kusema asilimia  95 za umeme zimekamilika na hadi kufikia kesho kutwa umeme utakuwa umewaka kwa asilimia 100 "

Kwa Upande wake Mhandisi  Musafiri Deudonne  muwekezaji kutoka itracom kutoka nchini Burundi ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwa na kasi ya katika kuhakikisha miundo mbinu inakuwa rafiki katika utendaji Kazi.

Deudonne ameipongeza TIC na Serikali na wadau wengine waliowezesha kufanikisha umeme na maji vinapatikana katika eneo la Nala kwani hiyo ndio ilikuwa changamoto kubwa kwa wawekezaji.

"Kasi imeonekana na sisi itracom tunaahidi kuanzia wiki ijayo tutakuwa tumeanza mradi wetu wa Ujenzi wa kiwanda cha  mbolea  lakini pia tunaahidi kuanzisha miradi mingine mingi"amesema Deudonne

 

 

Post a Comment

6 Comments

  1. Naomba lik ya kutuma maombi

    ReplyDelete
  2. Naomba mnisaidie link ya kutuma maombi kweny kiwanda cha mbolea dodoma

    ReplyDelete
  3. Naomba link ya kutuma maombi kwenye kiwanda cha mbolea Dodoma

    ReplyDelete
  4. Naomba link ya kutuma maombi ktk kiwanda Cha mbolea

    ReplyDelete
  5. Naomba link ya maombii

    ReplyDelete
  6. Tunaomben basi link tutume

    ReplyDelete