SERIKALI YAAHIDI USHIRIKIANO NA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU

 




📌MWANDISHI WETU

SERIKALI  imeahidi kuheshimu na kuzingatia mifumo ya  kulinda  haki za binadamu kwa mtu mmoja mmoja,makundi na Jamii kwa ujumla.

Hayo yalielezwa jana Jijini hapa na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi wakati wa kikao baina ya Wizara ya Katiba na Sheria  na Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu.

Prof Kabudi amesema kuwa  hiyo ni pamoja na kubuni na kutekeleza mikakati ya kukuza,kulinda na kutekeleza misingi ya haki za binadamu na wajibu wao.

Kama Serikali tuna jukumu pia la kuweka mazingira rafikio kwa wananchi kufikia vyombo vinavyo simamia haki katika ngazi zote,kulinda haki za Kikatiba za Wananchi wanaoshiriki katika mijadala mbalimbali inayohusus maendeleo ya Taifa lao na kutoa elimu kwa umma juu ya masuala ya Katiba na sheria ili kuimarisha  misingi ya kikatiba,demokrasia,utawala bora na utawala wa sheria.

Aidha alifafanua  Serikali imekuwa  inachukua hatua ya kupunguza mrundikano wa kesi Mahakamani ikiwa ni pamoja na kuimarisha  mfumo wa Wasajili wasaidizi katika Halmashauri zote ili kuwezesha uratibu na utoaji msaada wa kisheria katika masuala ya mirathi na ndoa.

“Hii ni katika kiuhakikisha huduma bora za Sheria zinapatikana kwa wakati na  gharama nafuu kwa kuongeza wataalam,miundombinu,vitendea kazi na kusogeza huduma karibu na wananchi ikiwa ni pamoja na kuimarisha Vyombo vya Sheria kwa kuongeza wigo wa huduma za utoaji wa haki nchini””,Alisistiza Profesa Kabudi.

Hata hivyo amesema Serikali  ipo tayari kushirikiana na Watetezi wa  Haki za Binadamu pamoja na  Wadau wengine wote wasio wa Serikali ambao wapo tayari kuunga mkono jitihada za Serikali za kukuza na kulinda  Haki za Binadamu na Watu.



Waziri Kabudi pia amesema Wizara yake itaendelea kushirikiana na wadau wa kutetea Haki za binadamu ili kuhakikisha wananchi wanapata haki  kama ilivyo ainishwa katika katiba na ilani ya Chama cha Mapindizi (CCM) 2020/2025.

 Tuko tayari kushirikiana na wadau ninyi muhimu kwenye masuala ya kupigania haki za wananchi tunajua kuwa mtakua na vipaumbele vyenu muhimu na serikali pia itakuwa na vipengele vyake  ambavyo vinalenga kukuza haki za binadamu  na kuleta maendeleo katika nchi yetu



Kwa Upande wake Mratibu wa Mtandao wa Onesmo Olengurumwa THRDC  alisema serikali inatambua kuwa mfumo bora wa sheria ndio msingi wa kutekeleza matakwa ya katiba,Sera,na mpango wa nchi.

Alisema asasi za kutetea haki za binadamu zimekuwa na mchango mkubwa kwa jamiii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata haki zao kwa wakati.

Asasi za kiraia zimekuwa zikifanya vizuri sana hapa nchini tunaomba serikali itambue mchango wa asasi hizo na kuongeza ushirikiano ili ziendelee kufanya vizuri kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla

Olengurumwa aliihakikishia serikali kuwa mashirika ya kutetea haki za binadamu yataendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha wananchi wanapata haki zao kwa wakati bila vipingamizi vyovyote.

Post a Comment

0 Comments