SERIKALI YAWATAKA WANANCHI KUTUMIA NISHATI MBADALA

 


📌JOHN BANDA

WAZIRI wa mifugo na uvuvi Mashimba Ndaki amewashauri wananchi kukubali kubadilika na kuingia kwenye matumizi ya nishati mbadala ili kuweza kukabiliana mabadiliko ya tabia nchi yanayosababishwa na uhalibifu wa mazingira

Pia amezitaka taasisi mbalimbali zinazojihusisha na utengenezaji wa nishati hizo kuwarahisishia wananchi upatikanaji wa uhakika pamoja na kuweka bei zafuu ambazo kila mtu atazimudu bila kujali hali yake

Waziri amesema hayo wakati alipotembelea maonyesho ya maadhimisho ya wiki ya mazingira yanayofanyika jijini Dodoma ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni  “tutumie nishati mbadala ili kuongoa mifumo ya Ikolojia” wakati alipokuwa katika banda la  Viridiam Tanzania LTD inayojihusisha na utengenezaji wa mkaa mweupe unaotengenezwa kwa kutumia majani

Ndaki amesema wananchi walizoea kulima, kufuga, kuvua bila tahadhari yoyote ya utunzaji wa mazingira lakini sasa inabidi wakubali mabadiliko kwa kufanya shuhuli zao hizo za kiuchumi kwa kutumia njia zinazoelekezwa na wataalamu

Alisema hata jikoni wengi wamekuwa wakitumia mikaa na kuni hivyo ili kuweza kulinda na kutunza mazingira ni vizuri watu wabadilike na kutumia nishati mbadala

Aidha alizitaka taasisi zinazojishuhulisha na nishati mbadala kuwakikishia wananchi upatikanaji wa uhakika pamoja na garama kuwa nafuu ili kurahisishia watanzania wote

Kwa mfano ninyi Viridiam Tanzania LTD hakikisheni mnakuwa na hifadhi ya kutosha mkaa huu mweupe ili kuwafanya watanzania waupate kiurahisi na bei iwe nafuu ili kila mtu aweze kuimudu.Kwa sasa mpo baadhi ya mikoa hakikisheni mnataka na kusambaa Tanzania nzima.

Mashimba Ndaki

Awali akitoa maelezo mbele ya waziri mifugo na uvuvi na ujumbe wake meneja masoko  wa Viridiam Tanzania LTD inayojihusisha na utengenezaji wa mkaa mweupe Aristle Nikitas alisema hivi sasa wanahifadhi ya zaidi ya tani laki nane za majani huku wakiwa na heka 75 za kilimo hicho huko chunya wakati iringa ziki 100,000

Nae meneja mauzo Abuu Habibu Ibrahimu amesema wanaziangatia ushauri wa serikali na kwamba wataufanyia kazi kwa kuangalia jinsi ya kupunguza bei toka bei ya sasa ya mkaa mweupe unaouzwa 2000 kwa kilo 2 na kuushusha zaidi

Aidha alisema kwa sasa wamejikita katika mikoa ya mbeya, Pwani, iringa, mwanza, na Dodoma ambapo kwa sasa wanaendelea kutoa elimu kisiwani Mafya na kwamba lengo lao ni kusambaza huduma hiyo nchi nzima

 

Post a Comment

0 Comments