BoT KUANZISHA MFUKO MAALUMU KUINUA SEKTA BINAFSI

 


📌HAMIDA RAMADHAN

BANKI kuu ya Tanzania ( BOT) inatarajia kuanzisha mfuko maalum wenye thamani ya shilingi Tilion 1 ambao utakaotumika kukopesha benki na taasisi za  kifedha kwa riba ya asilimia 3 ili taasisi hizo ziweze kukopesha kwa riba na nafuu ikiwa ni hatua mojawapo wa kuinua sekta binafsi ambayo imeonekana kusinyaa katika kipindi hiki cha ugonjwa wa UVIKO.

Akiongea na waandishi wa  habari wakati akitoa hatua za kisera za upatikanaji wa  mikopo binafs na kupunguza viwango vya riba Gavana wa  Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens  Luoga amesema Benki au taasisi ya kifedha itakayofaidika na mfuko huo itakayotakiwa kukopesha sekta binafs kwa riba isiyozidi asilimia 10 kwa mwaka. 

 

Hatua hii itaongeza ukwasi na kupunguza riba za mikopo kwa sekta binafsi

 Aidha amesema benki kuu imepunguza kiwango cha mtaji kitakachotumika kuwekwa na benki za biashara kwa ajili ya kuweza kutoa mikopo. 

 "Hatua  hii itasaidia kutoa fursa kwa benki za biashara kutoa mikopo zaidi kwa sekta binafsi kuliko ilivyokuwa hapo awali ." alisisitiza Profesa 

 Na kuongeza  kusema kuwa "Hatua hizi za kisera zimechukuliwa kwa mujibu wa sheria ya Benki kuu ya Tanzania  Sura. 197 na sheria ya mifumo ya malipo ya Taifa sura ya 437," amesema. 

Hata hivyo benki kuu imetoa unafuu kwa benki za biashara kwa kupunguza kiwango cha kisheria cha amana ambacho benki na Taasisi za kifedha zinatakiwa kuweka benki kuu, Ikiwa ni sehemu ya kutekeleza sera ya fedha. 

Prof.Luoga akiongea na Waandishi wa Habari katika
 ofisi za BOT jijini Dodoma

 Amesema  Nafuu hiyo itatolewa kwa benki itakayotoa mikopo kwa sekta ya kilimo kulingana na kiasi cha mkopo kitakachotolewa pia benki itakayonufaika itatakiwa kutoa mikopo kwa sekta ya kilimo kwa riba isiyozidi asilimia 10 kwa mwaka 

Hatua  hii inalenga kuongeza mikopo katika sekta ya kilimo na Kupunguza riba katika mukopo itakayotolewa 

Pia  ameeleza benki kuu ya Tanzania imeondoa Sharti la uzoefu wa kufanya biashara kwa angalau miezi 18 kwa Waombaji wa biashara ya wakala wa benki. 

 Amebainisha kuwa badala yake waombaji wa biashara ya wakala wa benki  wanatakiwa Kuwa na kitambulisho cha taifa au mamba ya kitambulisho cha Nida Ambapo hatua Hiyo itachangia kuongeza fedha katika mabenki kutokana na ongezeko la amana na kupunguza riba za mikopo.

Post a Comment

0 Comments