📌DOTTO KWILASA
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetoa mafunzo ya uelewa wa udhibiti wa masuala ya Nishati na Maji kwa Taasisi ya Maendeleo ya Viziwi Tanzania (TAMAVITA) huku ikiwa na matarajio kuwa semina hiyo itawasaidia kutimiza azma ya Serikali katika kuwasaidia watanzania kutambua haki na wajibu wao kwa jamii na kwa Serikali yao.
Mafunzo hayo yametolewa kwa Wananchama 60 ,ambapo 3o
kati yao ni wadau wa moja kwa moja kwa Mamlaka hiyo kwa kuwa na taaluma ya
mafundi umeme huku wakitegemewa kutoa huduma bora zaidi kwa jamii katika kukidhi
mahitaji ya ajira binafsi
Akizungumza leo Julai 20,2021 jijini Dodoma wakati
akifungua semina hiyo iliyoandaliwa na EWURA kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma, Anthony Mtaka , Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Dkt.Khamisi Mkanachi amesema
anaamini semina hiyo itawasaidia kutimiza azma ya Serikali katika kuwasaidia
watanzani kutambua haki na wajibu wao kwa jamii na kwa Serikali yao.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema , mojawapo ya majukumu
ya EWURA ni pamoja na kujenga uelewa kwa watumia huduma ili wafahamu haki na
wajibu wao.
Pamoja na hayo Dkt.Mkanachi ameitaka EWURA kuendelea
kujenga uelewa kwa watumiaji wa huduma mbalimbali ili wafahamu haki na wajibu
wao katika kuchochea maendeleo na kukuza uchumi.
“Ninafahamu kuwa ninyi ni sehemu muhimu yawatumia
huduma za EWURA,inawezekana kuna mafundi umeme humu ndani ambao inabidi wawe na
leseni ya EWURA vilevile inawezekana kuna wamiliki wa vituo vya mafuta ambao
inabidi wawe na leseni za EWURA au tunaweza kuwa na wamiliki wa kampuni za
kuzalisha na kusambaza umeme na sote tunatumia maji na umeme huduma ambazo
zinadhibitiwa na EWURA,”amesema
Amesema kwa niaba ya Serikali wanatoa shukrani za
dhati kwa Menejimenti ya EWURA kwa kukubali ombi la kutoa mafunzo hayo
kwani kwa kufanya hivyo wananchi wenye ulemavu wa kusikia watakuwa wanaelewa
shughuli za EWURA na mafundi umeme wataweza kutimiza matakwa ya kisheria na
kikanuni katika shughuli zao
Kwa upande wake,Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya
Maendeleo kwa Viziwi Tanzania (TAMAVITA) Bw.Kelvin Nyema,amesema kuwa
chama chao kimefikia hatua ya kuomba kupatiwa mafunzo hayo ili wajengewe uwezo
mafundi umeme na mafundi wa nyumba ambao ni viziwi.
“Miongoni mwa viziwi wapo mafundi wa umeme, mafundi ujenzi wa nyumba na tunajua tunahitaji leseni lakini hatujui nini cha kufanyeje, pia viziwi ni watumiaji wa maji na nishati na ndio maana tunahitaji mafunzo,”amesema
Awali akiwasilisha mada,Meneja Mawasiliano na
Uhusiano EWURA,Titus Kaguo ameeleza kuwa Mafunzo hayo yametolewa kutokana na
uongozi wa TAMAVITA kuomba kupewa elimu na uelewa wa masuala ya udhibiti wa
nishati na maji hali itakayolenga zaidi kuchochea maendeleo.
Kwa umuhimu huo Kaguo amezishauri Taasisi nyingine
kuona umuhimu wa kutoa mafunzo kwa makundi maalumu ili kuleta hamasa kwa jamii
kuwasaidiakatikakutekeleza majukumu ya uzalishaji na kujiiunua kiuchumi.
“Nazishauri Taasisi nyingine kutowaacha wenzetu hawa
ambao wanaonekana kama ni watu wa pembeni waliosahaulika kwani nao wana uwezo
wa kutumika kujenga uchumi wan chi yetu,”amesisistiza Meneja huyo wa
EWURA.
Pamoja na mambo nengine ameongeza kuwa hatua hiyo ya
mafunzo imekuja kwa kuzingatia kuwa kundi hilo ia ni wadau muhimu kwa Taasisi
hiyo ambapo kati ya Wananchama hao 60 ,3o kati yao ni wadau wa moja kwa moja
kwani wana leseni za Ewura hivyo.
“Na kwa kuwa hapa tuna mafundi umeme 30 basi
tunategemea huduma bora zaidi kutoka kwenu na kuongezeka kwa ajira
binafsi,tumetimiza wajibu wajibu wetu kuwajenga na kuwaelimisha ili wawe
mabalozi kwa wenzao,jamii imekuwa na tabia za kuwasahau wenzetu wa makundi
maalum kwa kufanya hivi itasaidia makundimaalumu kuheshimika na kushirikishwa
katika uchumi wa viwanda,”amesema
0 Comments