📌ZUENA
MSUYA
WAZIRI
wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani amesema Serikali itajenga kituo kikubwa cha
kupoza Umeme katika Wilaya ya Kongwa ili kumaliza tatizo la kukatika umeme mara
kwa mara na kuboresha upatikanaji wa Umeme katika wilaya hiyo na maeneo
jirani.
Dkt.
Kalemani alisema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miundombinu ya
umeme ikiwa ni pamoja na kutembelea eneo litakalojengwa kituo hicho lililopo
katika Kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni Wilayani ya Kongwa mkoani
Dodoma,Julai 27,2021.
Katika
ziara hiyo, Dkt. Kalemani alisema kuwa tayari eneo la ukubwa wa Hekari 130
limepatikani ambalo litatumika kujenga kituo hicho, kitakachokuwa na uwezo wa
kufua umeme wa Kilovolti 220.
Aidha
alisema kuwa tayari zaidi ya shilingi milioni 63 zimetengwa kwa ajili ya
kuwalipa fidia wakazi wa eneo hilo watakaopisha Ujenzi wa Mradi husika ambao
utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 41.2.
Ujenzi
wa kituo hicho unatajia kuanza kutekelezwa mapema mwezi Septemba mwaka huu
2021.
“Tuna
umeme mwingi sana Mkoa wa Dodoma, lakini kuna changamoto kubwa kukatika umeme
na wenye nguvu ndogo katika maeneo yote ya Wilaya ya Kongwa, kwa kipindi cha
miaka mingi sana, hii inatokana na umeme huo kusafiri umbali mrefu kutoka kituo
cha Zuzu hadi kufika huku takribani kilomita 120 na mzunguko ni takribani
Kilomita 2000, suluhisho la kudumu ni ujenzi wa kituo cha kufua umeme ambacho
kitamaliza kabisa tatizo hilo na kuwa historia, hasa katika Viwanda,
Wafanyabiasha na watumiaji wengine”, alisema Dkt. Kalemani.
Hata
hivo alisema kuwa, katika kutatua tatizo la kukatika Umeme mara kwa mara katika
maeneo ya Mbande, Kibaigwa, Kongwa, Mpwapwa na Kiteto, ndani ya wiki hii
kitafungwa kifaa maalum, kinachojulikana kama AVR ili kuuongeza nguvu ya Umeme
katika maeneo hayo.
Dkt.
Kalemani alifafanua kuwa kifaa hicho tayari kimeshatoka mkoani Ruvuma kuja
Dodoma na kufungwa katika eneo la Mbande.
Sambamba
na hilo kazi ya Ujenzi wa Njia ya kusafirisha Umeme wa kV 220 inaendelea
kujengwa kutoka Zuzu kupitia Mpunguzi hadi kufika wilayani humo ili kupunguza
tatizo la kukatika kwa Umeme mara kwa mara katika maeneo tajwa na mengine
jirani.
Ujenzi wa njia hiyo ya umeme umefikia zaidi ya 55%.
Kufuatia
utekelezaji wa miradi hiyo, aliwataka wakazi wa maeneo hayo kuvuta subira
wakati tatizo la kukatika Umeme na kusambaza Umeme katika maeneo ambayo
hayakufikiwa likitatuliwa hivi karibu.
Aidha
aliweka wazi kuwa kuanzia mwaka wa fedha ujao, mkoa wa Dodoma utagawanywa
Kitanesco na kuwa kama majiji mengine ikiwemo Dar es Salaam kwa lengo la
kuimarisha na kuboresha huduma za umeme kwa wateja.
Vilevile
alitumia ziara hiyo kukipandisha hadhi kituo cha umeme cha Kibaigwa kuwa kituo
cha Wilaya ili kuimarisha na kuboresha upatikanaji wa umeme katika maeneo hayo.
Akizungumzia
suala la usambazaji wa umeme vijijini, Dkt. Kalemani alimtaka mkandarasi
kuongeza kasi katika kutekeleza kazi hiyo na kwamba wananchi wote waliolipia
waunganishiwe umeme kwa wakati.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka aliwataka wakazi wa eneo
litakalolegwa kutuo cha kupoza umeme kuwa walinzi wa kituo hicho na kutoa
ushirikiano kwa watakaotekeleza kazi hiyo.
Vilevile
aliwataka wakazi wa maeneo ambayo bado hayajafikiwa na umeme kujiandaa kuupokea
umeme huo kwa kutandaza nyaya katika nyumba zao pamoja na kulipia ili kuwa
tayari kuunganishiwa umeme.
Mkoa
wa Dodoma unawakandarasi 3 ambao watakaotekeleza mradi wa kusambaza umeme
katika vijiji vyote vilivyosalia kwa kipindi cha miezi 12 na kwa gharama ya
shilingi 27,000 tu.
Mkoa
wa Dodoma kwa sasa unaongoza kwa kuwa na megawati zaidi ya 640 za umeme
ukifatiwa na mkoa wa Dar es Salaam wenye megawati zaidi ya 500.
0 Comments