MAADILI NDIO IWE MSINGI WA KAZI ZENU- DKT. MAGEMBE

 

📌ASILA TWAHA

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt. Grace Magembe  amewataka wafamasia kufuata maadili ya kazi zao ili kulinda heshima katika kada husika.

Dkt. Magembe ameeleza hayo katika ufunguzi wa mafunzo ya usimamizi na udhibiti wa bidhaa za Afya kwa wafamasia wa Mikoa na Halmashauri  Julai 28, 2021 Jiji Dodoma.

Amesema wafamasia ni moja kati ya kada muhimu katika sekta ya afya ambayo inahitaji watendaji waadilifu na wenye uaminifu  katika kutekeleza kazi zao.

 "Wapo baadhi ya wanataaluma wachache wasio waadilifu na wanaharibu kwa kutokuwa waaminifu na kuharibu taaluma hiyo ambayo inategemewa katika  mchango mkubwa kwenye Sekata  ya Afya.  Amesema Magembe, nakuongeza

hata tukinunua dawa kiasi gani lakini kama hakuna usimamizi mzuri hatuwezi kupiga hatua

Katika hatua nyingine, ameweka wazi  na kutoa maelekezo kupitia mafunzo hayo kwakuwataka wataalam wote wa Afya  kuzingatia  taratibu za serikali  katika usimamizi wa bidhaa za afya na  pale itakapobainika  kuwepo na uzembe  au ubadhilifu wa ukiukwaji wa taratibu, kisheria na kanuni ambazo zinaisababishia serikali kupata hasara  hatua kali zitachukuliwa. Amesisitiza

Ni jukumu la kila mmoja wetu aliyepo  hapa kuhakikisha kuwa jamii inapata huduma bora za dawa kulingana na miongozo ya tiba iliyopo

Dkt. Grace


Vilevile amewawataka wakaguzi na maduka ya dawa kuwa na wajibu wa kutoa taarifa kwa Baraza na mamlaka wanazoshirikiana nazo wakiwemo Mamlaka ya Chakula na Dawa (TMDA) kuhusiana na ukiukwaji wa sheria, kanuni na miongozo inayohusiana na utoaji wa huduma na utendaji wa taaluma iwe kwenye sekta binafasi au ya umma

Naye Masajili wa Baraza la Famasi nchini Bi. Elizabeth Shekalaghe ameishukuru serikali kwakuongeza bajeti ya Afya na kuwahimiza wafamasia kusimamia maadili na kuipenda kazi yao kwa kujitoa kuitumikia vyema taaluma yao.

Post a Comment

0 Comments