MIFUMO YA CHAKULA NI FURSA YA AJIRA KWA VIJANA-PROF.MWAMFUPE



📌 MWANDISHI WETU

VIJANA wa Tanzania wanayo fursa kubwa ya kuchangia kwenye kutatua changamoto za mifumo ya chakula kwa kutumia ubunifu, ujuzi na maarifa.

Ushauri huo umetolewa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe wakati akifungua kongamanao la vijana kujadili mifumo ya chakula (Food System Summit) kwa mwaka 2021 mkoani Dodoma.

Amesema suluhisho la uhakika wa mifumo ya chakula unategemea sana ubunifu na ushiriki wa vijana nchini ili sekta ya kilimo iwe endelevu na kuzalisha ajira kwa vijana wanaojihusisha kwenye mnyororo wa thamani katika sekta ya Kilimo ..

Kwa upande wake Mshauri wa Sera na Mratibu wa Mkakati wa Vijana kushiriki kwenye Kilimo toka Wizara ya Kilimo Revelian Ngaiza alisema mkakati wa serikali unahusisha kuwajengea uwezo vijana kuanzisha Kilimo biashara na kuajili wengine ili kuchangia zaidi kwenye uchumi wa Taifa.



Serikali inawataka vijana nchini kupitia kongamano hili  watoe mawazo katika kuboresha mifumo ya chakula itakayochangia kukuza uchumi wa vijana na taifa kupitia sekta ya Kilimo
Ngaiza.

Akitoa mada kwenye kongamano hilo Mtaalaam wa lishe kutoka Wizara ya Kilimo Magret Natai alisema Mifumo ya Chakula inamaanisha kuwa “mkusanyiko wa shughuli mbalimabali zinazohusisha uzalishaji wa chakula, kuanzia kwa mzalishaji (mkulima na mfugaji) ukijumlisha wadau wa kati, wasambazaji ,wasindikaji, wasafirishaji mpaka mlaji” .

Naye  mtaalam wa lishe kutoka Shirika la Mpango wa Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) Stella Kimambo akichangia kwenye kongamano hilo amesema kuna umuhimu wa kubadili utaratibu wa uzalishaji na matumizi ya ulaji vyakula vyenye kuzingatia lishe bora .

Wizara ya Kilimo imepewa jukumu la kuratibu na kuhakikisha wadau wote wa sekta ya umma na binafsi katika mfumo wa chakula wanashiriki mijadala ambapo mapendekezo ya nchi yatawalishwa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika mwezi Septemba mwaka huu New York Marekani.

                                                                          

Post a Comment

0 Comments