📌FAUSTINE GIMU GALAFONI
WAZIRI mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Kayanza Peter Pinda amelishauri Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali[NaCONCO ]kuwa daraja la kusaidia vijana kuwaelimisha ili wajitambue kuwa wao sio taifa la kesho bali ni taifa la leo na wachangamkie fursa za kilimo na ufugaji.
Mhe.Pinda amebainisha hayo nyumbani
kwake kijijini Zuzu Mkoani Dodoma alipotembelewa na
wajumbe wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali [NACONGO] lengo ni
kujifunza namna alivyowekeza katika sekta ya kilimo na ufugaji.
Waziri mkuu mstaafu huyo amesema vijana
wana nafasi kubwa katika mchango wa taifa hivyo wanatakiwa kuchangamikia fursa
zinazowazunguka hususan sekta ya kilimo na kubainisha kuwa kuna haja ya kuwa na
kituo cha kilimo kila kanda hali itakayochochea zaidi vijana kujikita
katika sekta hiyo.
"Kwa takwimu zilizopo kundi la hawa
vijana ni kubwa sana ,kikubwa ambacho mnatakiwa kukiangalia ni kuwaangalia hawa
vijana kwa mawanda mapana kundi la vijana ambao hawakusoma na vijana
wasomi,ukitaka kuwasaidia vijana lazima uangalie unafanyaje,ushauri wa kwanza
tujaribu kuwaasa vijana wajitambue kuwa wao sio taifa la kesho bali ni taifa la
leo ,yote na yote kama kijana lazima uangalie fursa zinazokuzunguka hivyo ninyi
NACONGO mnatakiwa muwe daraja la kuwaelimisha vijana wachangamkie fursa hasa
kilimo’’amesema.
Kuhusu asasi za kiraia husan Baraza la Taifa
la Mashirika yasiyo ya Kiserikali [NACONGO]Mhe.Pinda amesema zina mchango
mkubwa kwa maendeleo ya jamii hivyo amewaasa kuwa mstari wa mbele pia katika
kuelimisha jamii kuondokana na hali ya utapiamlo nchini pamoja na
mapambano dhidi ya umasikini.
Aidha,Waziri mkuu mstaafu huyo
ametoa wito kuwa na uwazi masuala ya kifedha kwa asasi za kiraia ili
ziweze kuaminika zaidi kwa serikali.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali Lilian Badi amesema hatua ya ziara hiyo wamejifunza mengi kuhusu masuala ya kilimo huku akitoa ombi la kuwezeshwa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya NACONGO.
“Sisi kama wajumbe wa NACONGO tumefarijika
sana tumezunguka katika mashamba mbalimbali ikiwemo maeneo ya
zabibu,miembe,ufugaji wa samaki ,nyuki hakika tumejifunza mengi kwa busara
zako,kama wewe mtu mkubwa serikalini unakubali kukaa shambani ,iweje sisi
vijana tulinge tukimbilie mjini hongera sana mzee wangu,pili sisi hatuna ofisi
tunachohitaji kiwanja hakika tukipata kiwanja tukajenga ofisi ya kudumu hapa
makao makuu ya nchi ,Dodoma kuliko kuishi nyumba ya kupanga Dar Es Salaam
hakika NACONGO itaendelea fedha za kujenga ofisi hatutakosa tukipata kiwanja
tutajitutumua “amesema.
Mtoto wa Waziri mkuu Mstaafu ,Peter Pinda
amewaasa watanzania kuondoa dhana potofu kuwa kilimo ni umasikini.
Vijana tunachotakiwa ni kubadilika tuachane na dhana potofu kuwa kilimo ni watu waliokosa kazi tulime
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la
Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali [NaCONGO]akiwemo Novatus
Marandu kutoka mkoani Kagera,Penina Manyanki kutoka Dodoma ,Musa Ngangala
kutoka Shinyanga ,Angelus Tungaraza kutoka Kigoma ,Stambuli Shemkomba
kutoka Lindi pamoja na Gaidon Haule kutoka mkoani Pwani wamesema kupitia
ziara hiyo wamejifunza mengi na kuahidi kwenda kueneza ujumbe kwa
vijana fursa za kilimo.
Shamba la Waziri Mkuu Mstafu Mizengo Pinda
linajumuisha miradi mbalimbali ikiwemo kilimo cha zabibu,kilimo cha
miembe,kilimo cha nyanya ,ufugaji wa ng’ombe,na ufugaji wa nyuki .
0 Comments